Vitate

Vitate ni maneno ambayo matamshi yake yanakaribiana lakini maana ni tofauti.

Mifano ya vitate

 • vua – toa nguo

 • fua – osha nguo

 • jaa – mahali pa kutupia takataka
 • njaa – hali ya kuhisi kutaka chakula

 • wasaa – muda

 • fursa wasa – toa nasaha

 • nyusi – nywele za paji la uso
 • nyuzi – digrii

 • pishi – chombo cha kupimia nafaka

 • bishi – enye kupenda ugomvi

 • kata – lokesheni                                 

 • kataa – kutokubali

 • posa – ombi la kutaka kuoa                            
 • poza - malipo ya kumtuliza mtu

 • paa – enda juu                        

 • baa – janga

 • bahasa – sio ghali                      

 • bahasha – karatasi  ya kutia barua

Mifano ya vitate

 • ugua – pata ugonjwa
 • ungua – teketea, chomeka
 • kula – kupata mlo             
 • kura – uchaguzi

 • mandari – matembezi ya kujistarehesha
 • mandhari – sura ya nchi
 • kaburi – shimo la kuzikia maiti
 • kabuli – wali wa pilau ya papa au nguruwe
 • kaba – bana kwa nguvu            
 • kamba – uzi mnene
 • piga – chapa
 • pinga – kutokubali
 • mkembe – mtoto
 • mkebe – chombo cha kuwekea vitu

 • samani – fanicha
 • zamani – kale

 • koma – kuacha kufanya jambo
 • komaa – kuwa kubwa, kupevuka
 • mchi – mti wa kutwangia vitu kwa kinu
 • mji – makazi ya watu wengi

Mifano ya vitate

1. sisi – nafsi ya kwanza wingi
zizi – makao ya ng’ombe   

2. pofu – asiyoona
povu – vipotopoto vya hewa  

3. zabuni – uza kwa kushindania bei
sabuni – mchanganyiko  wa kufulia na kuoge

4. sabiki – kuwa mbele, tangulia
shabiki – mtu apendaye jambo au kitu sana

5. lila – wema
lira – aina ya pesa

6. jibu – jawabu. Neno la kuitikia au kujibia  
jipu – uvimbe mkubwa wenye usaha

7. acha – tengana na mtu, hali au kitu
asa – kanya, shauri

8. shati – vazi
sharti – lazima

9. mjuzi – mwenye ujuzi
mjusi – ugonjwa wa kutoka damu puani;

10. manda – kitu kinachoweza kushikika
mada – kiini cha jambo fulani

11. ndugu – Watoto wa ukoo mmoja 
dungu – sehemu anayokaa rubani

12. taga – toa yai katika kiloaka 

 

tagaa – tawi

 

13. nyati – aina ya mnyama wa porini
nyeti – enye ugumu

14. machi – mwezi wa tatu wa mwaka
mechi – mashindano ya mchezo.

15. sahibu – rafiki

 

 

 

shaibu – mzee mwanamume

 

16. tosa – tia kitu katika kitu kiowevu.
toza – kiko, chombo cha kuvutia tumbako

 

17. machozi – Matone  yatokayo machoni 

 

majonzi – hali ya kutokuwa na furaha.

 18. bunge – Baraza la taifa la kutungia sheria

 

buge – Mtu aliyekatika kidole

 

19. ngeli – mpangilio wa makundi ya nomino

geli – mchezo wa watoto wa kurusha vijiti


20. shairi – mtungo wa kisanaa wenye mpangilio maalum 

shahiri – Waziwazi 

shayiri – Aina ya nafaka • bahasha by Original Wavelength used under CC_BY-SA
 • digrii by Hide-E-Hole used under CC_BY-SA
 • njaa by pinterest used under CC_BY-SA
 • Paa by Galaxy dreams used under CC_BY-SA
 • Posa by Madame Noire used under CC_BY-SA
 • Saa by Northern Illinois University used under CC_BY-SA
 • fanicha by maincpamek used under CC_BY-SA
 • Mtoto by pinterest used under CC_BY-SA
 • Piga-kura by Jambonewspot.com used under CC_BY-SA
 • vi10 by Kenya advisor.com used under CC_BY-SA
 • vi11 by www.acne.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • vi13 by commonmwanachi.blogspot.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • vi14 by fullskyart.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • vi111 by www.indiamart.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • vit222 by https://www.pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • vit333 by amazingworldfactsnpics.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • vit444 by www.africanews.com & eLimu used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.