Maswali kadirifu

Maamkizi

Jibu maamkizi yafuatayo kwa usahihi.

1. Sabalkheri ni salamu za wakati gani?____.

2. Utamjinuje mtu akikuamkia,'salaam aleikum'

3. ' Tutaonana kesho kutwa', nilimwahidi rafiki yangu. Alinijibu ____.

4. Mjukuu atamwamkiaje babu yake wakikutana?____.

5. Masalkheri ni salamu za wakati gani?____.

6. Jibu sahihi la masalkheri ni ____.

7. Upendo alimsabahi Tina,' Habari za asubuhi', naye Tina akamjibu ____.

8. Toa jibu sahihi la salamu,habari za kutwa?____.

 9. Jibu la salamu,alamsiki ni ____.

10. Mtangazaji aliwaaga watazamaji wa runinga lwa maamkizi, 'Laleni salama. 'Taja jibu la salamu hizi.____

11. "Nakutakia usingizi mwema',

11. 'Nakutakia usingizi mwema,' Dan alimwambia mwenzake. Alijibiwa ____.

12. Taja jibu la salamu, usiku mwema.

13. 'Muwe na ndoto njema',Chausiku alituaga nasi tukamjibu ____

14. Mtu akikwambia',Lala unono'utamjibu ____.

15.'Hujambo kaka',nilimchangamkia rafiki yangu.Hakusita kunijibu ____.

Abadu na heshima

 1. Kevin alipompata mama yake akizungumza na jirani, badala ya kudakiza alisema ____.
 2. Nilipoupita mtihani wa taifa , shangazi alinipongeza kwa kuniambia ____.
 3. Ukitaka mtu akupishe njia utamwambia ____.
 4. Nilipofika mekoni, mpishi aniitilia mshumbi wa wali nami nikasema _____.
 5. " _____ mumuchangie hela kipofu huyu ajiendeleze kimasomo", kasisi aliwahimiza waumini. Taja neno adabu alilotumia.
 6. Mtangazaji wa habari alisema _____ baada ya kusoma neno isivyostahili
 7. Shangazi yetu Jasmin alipofariki tuliambia jamaa yake ____.
 8. Safari ya kuelekea Ulaya ilikuwa imepangwa ikapangika.Nilimwambia rafiki yangu tungefika salama ____.
 9. ____ Mzee Jomo Kenyatta alikuwa rais mwenye hekima.
 10. ____ na ____ arusi walikuwa wamejikwatua kwatukwatu siku hiyo.
 11. ____ babu yangu alipenda sana kunitambia hadithi za mazimwi.

Methali

A. Kamilisha methali zifuatazo.

1. Jifya moja _____.

2. Subira in ufunguo wa _____.

3. Asiye na mwana aeleke _____.

4. Ng'ombe akivunjika mguu malishoni _____.

5. Sisimizi hawi _____.

6. Mwiba wa kujichoma _____.

7. Mshale mzuri _____.

8. Mchuma janga _____.

9. Mcheza kwao _____.

10. Sanda ya mbali _____.

11. Bahari haaishi _____.

12. Alisifuye jua _____.

13. Pendo zake mwana _____.

14. Ganga ganga za mganga _____.

15. Uta wa mshindi _____

16. Mdharau biu _____.

17. Imara ya jembe _____.

 

B.Toa methali zingine  zenye maana sawa na hizi

1. Dunia ni msumeno hukata mbele na nyuma.

2. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.

3. Polepole ndio mwendo

4. Njia mbili zilimshinda fisi.

5. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.

6. Mchumia juani hulia kivulini

7. Haba na haba hujaza kibaba.

8. Usipoziba ufa utajenga ukuta.

9. Fimbo ya mbali haiuwi nyoka

10. Baniani mbaya kiatu chake dawa

 

C. Eleza maana ya methali hizi:

 1. Mtegemea nundu haachi kunona.
 2. Mpanda ngazi hushuka
 3. Heri nusu shari kuliko shari kamili.
 4. Wagombanao ndio wapatanao
 5. Ajali haina kinga wala kafara
 6. Aisifuye mvua imemnyea.
 7. Dau la mnyonge haliendi joshi
 8. Wanja wa manga si dawa ya chongo.
 9. Hujafa hujaumbika.
 10. Zingwizingwi lipe nguo,ulione mashauo.

D. Andika methali zinazotumia majina haya:

1. punda

2. paka

3. kuku

4. ng'ombe

5. mbwa

6. nguruwe

7. simba

8. ndovu

9. kobe

10. papa

Kinyume

A. Taja vinyume vya maneno haya.

 • njaa
 • vita
 • kutwa
 • machweo
 • faragha
 • ufu
 • mbingu
 • kigongo
 • rasi
 • pwani

 

B. Taja vinyume vya kufanyua

 1. choma
 2. bana
 3. ziba
 4. pakia
 5. chimba
 6. pamba
 7. tia
 8. jenga
 9. umba
 10. kama

Wizara

Jibu maswali haya kwa usahihi.

1. Ni wizara gani itashughulikia masuala kama kuzuka kwa magonjwa na utoaji chanjo? _____.

2. Ni wizara gani nchini inayohusika na spoti? ____

3. Ni wizara gani inayohusika na makadirio ya ngwenje ?____

4. Mimi nataka kumiliki pasipoti ili nizuru mataifa ya kigeni. Je, ni wizara gani itakayonisaidia ?_____

5. Ni nani kiongozi wa vitengo vifuatavyo:

a) Wizara

b) idara

6. Bainisha taasisi na asasi,kaimu na makamu.

Ushairi

A. Jibu maswali yafuatayo kuhusu ushairi.

1. Ushairi ni nini?

2. Shairi ni nini ?

3. Silabi kayika mashairi huitwa _____

4. Shairi la tarbia lina mishororo mingapi katika kila ubeti?

5. Mshororo wa kwanza katika shairi huitwaje?

6. Mshororo wa pili katika shairi unaitwa _____.

7. Mshororo wa pili  katiak shairi unaitwa _____.

8. Shairi lenye vina vinavyofanana kutoka ubeti wa kwanza hadi ule  wa mwisho linaitwa _____.

9. Shairi lenye mishororo kumi katika kila ubeti huitwa ____.

10. Mashairi ya tarbia huwa na vipande  vingapi?

 

B. Soma ubeti huu kisha ujibu maswali yanayofuata.

Anita nakueleza , jambo bora ni elimu,

Yalo mema tekeleza ,yasemwayo na walimu,

Jaribio tekeleza, kwa alama kemukemu,

Alo na chungu mekoni , haishi kuriyariya.

 

 1. Kifungu hiki cha shairi kinaitwaje?____.
 2. Kifungu hiki kina jumla ya mizani mingapi?_____.
 3. Onyesha vina vya kati na vya mwisho. _____.
 4. Shairi hili lina vipande vingapi ?
 5. Shairi hili ni la aina ya _____.

Tanakali za sauti

Jaza sentensi zifuatazo kwa tanakali sahihi.

1. Jambazi lilipigwa kipopo,likaanguka na kunyooka _____.

2. Mafadhali wale walipopigana, wote walianguka penye mwamba _____.

3. Msasi alikabiliana na chui mkabala. Wakapigana na kuanguka mchagani _____.

4. Ali aliteleza _____ topeni.

5. Mtemakuni alipolichupia tawi,lilikatika naye akatumbukia majini _____.

6. Mwalimu Muroki alichekwa na wanafunzi alipotoa sarafu chache mfukoni. Zilianguka sakafuni _____.

7. Babu alirushia jambazi kibago . Kikamkosa na kupiga ukuta wa nyumba,kikavunjika _____.

8. Wageni hao walikuwa wametayarisha mchuzi _____.

9.Mama ana matatizo _____.

10. Jana nilichoka  _____ baada ya kuandika insha tatu.

Istiara

Eleza maana ya istiara zifuatazo

 1. Kijana yule wa mzee Pepto ni sungura ._____.
 2. Ngumi za mwanandondi Suleiman Bilali ni mawe .____.
 3. Bibi Almasi siku hizi ni tausi ._____
 4. Jengo la babu yetu ni mwamba .____.
 5. Otieno ni kizimwili,akiwa gizani hatambuliki. _____.
 6. Ndugu yake Taffari amekuwa jeta._____.
 7. Binamu yangu huchekwa na wenzake kwa kuwa yeye ni samaki. ____.
 8. Amiri Jeshi Songambele ni shetani. _____.
 9. Ngozi ya dada yangu Miriam ni pamba _____.
 10. Mwanariadha Kiprotich ni korogo._____

Maswali

1.Kamilisha methali :-

Amani haipatikani kwa ncha ya  ______.

A. mkuki    B. kisu

C. mshale   D.

 

2. Upanga tunasema mlariba ilihali mtambaa huambatanisha na _____.

 A. panya   B. mwana

 C. milia    D. njia

 

3. Tegua kitendawili hiki:

Faiza akiniona ajificha.

A. Kobe

B. Mwezi

C. Kivuli

D. Kinyonga

 

4. Baada ya kupika pure mama alienda _____mikate.

A. kuchemsha

B. kuoka

C. kukaanga

D. kubainika

 

5. Wanaume waliooa dada wawili kutoka nyumba moja wanaitanaje?

A. Marvyaa

B. Mitara

C. Mwamu

D. Mwanyumba

 

6. Chagua kifungu kilicho tofauti na vingine.

A. Alamsiki - Binuru.

B. Buriani - Buriani dawa

C. Pole - Asante

D. Hujambo - Sijambo