Maamkizi

Maamkizi / maamkio / utweshi

- Maamkizi hutumika kujuliana hali.

- Ni maneno ya kuamkiana. Kuna maamkizi yanayoweza kutumika nyakati zozote na baina ya watu wowote.

- Mengine hutumika mnamo nyakati maalum.

 

Maamkizi na Majibu

1. Habari? - njema/nzuri

2. Uhali gani? - njema/nzuri

3. Je la utu? - sina utu

4. Waambaje? - sina la kuamba/salama

5. Sabalkheri? - sabalkheri/aheri

 

6. Masalkheri? - masalkheri/aheri

7. Alamsiki? - alamsiki binuru

8. Shikamoo/ - marahaba / kuzinawe nashikamoo?

9. Chewa? - chewa

10. Salaam aleikum - aleikum salaam

 

11. Buheri - buheri afya

12. Buriani - buriani dawa

13. Hujambo? - sijambo

14. Umeshindaje? - salama

15. Umeamkaje? - salama

 

16. Habari za kutwa - njema/nzuri

17. Hongera kwa - asante nimehongea ushindi

18. Pole kwa ugonjwa - asante nimepoa

19. Lala salama - pia nawe / wa salimini

20. Kwaheri ya kuonana - kwaheri ya kuonana

 

21. Tuonane tena - Inshallah / Mungu akipenda

22. Makiwa - asante tunayo / asante yamepita

23. Karibu tule - starehe

Muhtasari

a) Wakati wowote                            

  • Habari?                Nzuri                                    
  • U hali gani?          Njema                               
  • Waambaje?          Sina la kuamba                             
  • Hujambo?            Sijambo                               
  • Shikamoo?           Marahaba 

b) Asubuhi                                  

  • Sabalkheri?             Aheri
  • Umeamkaje?           Salama 
c) Wakati wa jioni
  • Umeshindaje?            Salama
  • Masalkheri?             Aheri
d) Kuagana
  • Kwaheri ya kuonana          Kwaheri ya kuonana.
  • Tuonane tena                     Majaliwa

 

Unadhani huu ni wakati gani?

 

e) Usiku

  • Lala unono              Pia nawe
  • Alamsiki                   Binuru

 

f) Umri

Ni nini inafanyika kwenye picha hii?
 
 
Bidii: Shikamoo?
Mjomba: Marahaba Bidii! Uhali gani?
Bidii: Njema. Nimefurahi kukuona (Huku akitabasamu. Amekumbuka jinsi mjomba huwaletea maembe dodo matamu matamu). 
Mjomba: Nami pia. Habari za nyumbani?
--- (Tathmini na uendeleze)
 
  • Toa majibu ya maamkizi haya.
i) Shikamoo?  
ii) Wambaje? 
iii) Alamsiki 
iv) Habari za utokako? 
v) Tuonane kesho