Vitendawili

- Kitendawili ni maneno yanayoficha kitu au jambo ili lisijulikane kwa urahisi. Kitendawili hulinganisha hali fulani na jambo jingine.

- Kitendawili humpatia mwanafunzi nafasi ya kuchemsha bongo na kulinganisha hali moja na ile nyingine.

 

Tegua vitendawili vifuatavyo.

1. Akiondoka hatuonani.

2. Wanashindana wakifuatana.

3. Wanashinda wakifuatana.

4. Huku ng’o na kule ng’o.

5. Huku mwamba na kule mwamba.

6. Mombasa kwametameta.

7. Amefunika dunia kwa blanketi jeusi

8. Amefunua jicho jekundu.

9. Saa yangu haijalala.

10. Nyumba yangu ya nguzo moja tu.

11. Nyumba yangu isiyo na mlango.

12. Ametaga yai mibani.

13. Nne amekalia nne akimsubiri nne.

14. Popoo mbili zavuka mto.

15. Ninaye ng’ombe wangu ambaye hafanyi kazi nisiposhika mkia.

16. Nikitoa machozi watu hunufaika.

17. Mlangoni mwangu mna askari.

18. Mkufu usiofungika shingoni.

19. Bak bandua bak bandika.

20. Nikiitana huitana, nikiitika huitika.

21. Kiti cha dhahabu kisichokalika.

22. Likitoka halirudi.

23. Kutoa ni kuongeza.

24. Wanaingia wakitoka.

25. Akikasirika mvuvi hunufaika.

26. Safari isiyo marejeo.

27. Mlimani sipandi.

28. Halemewi kubeba.

29. Mama nieleke.

30. Ubwabwa wa mwana mtamu. 

31. Shamba langu kubwa lakini mavuno hayajai ukufi.

32. Njoo ukamwone umpendaye.

33. Tik! Tik! Kucha kutwa!

34. Ni mgeni wa kila mtu lakini huleta huzuni.

35. Hujilinda bila silaha.

36. Aliwa, yuala, ala, aliwa.

37. Ni mdogo lakini humaliza gogo.

38. Ukoo wetu hatuishi safari.

39. Atolewapo majini hufa.

40. Hutumbuiza watu kwa nyimbo huko msituni.