Tashbihi jozi

- Tashbihi jozi hutumika kufananishia katika hali ya kutendeana au kutendana. Katika hali hii, nomino mbili huwa zinatendeana au zinatendana.

- Hivyo basi, tunafananishia vitendo vyao na jozi k.m. Watu wawili wanapopendana (hali ya kutendana) tunaweza kufananisha kupendana kwao na kule kwa chanda na pete.

 

Mifano

1. Wanafunzi wale wanashirikiana curriculumni kama kinu na mchi, kiko na digali.

2. Tabia za ndugu hao wawili zinatengana kama ardhi na mbingu.

3. Daima dawama watoto wale huwa pamoja kama ulimi na mate.

4. Urafiki wa jirani hao ni ule wa uta na upote, chanda na pete.

5. Daima mume na mkewe yule hufuatana kama mtu na kivuli chake.

6. Wao wanafanana (wanalandana) kama Kurwa na Doto; maziwa na tui; shilingi kwa ya pili; reale kwa ya pili: rupia kwa ya pili.

7. Chukiana kama maji na mafuta.

8. Elewana kama mume na mke.

9. Wao wanategemeana kama viungo vya mwili.

10. Mikakati yao imetofautiana kama giza na mwangaza, usiku na mchana.

11. Hawaaminiani. Wamekuwa kuku na mwewe.

12. Mambo yao yanalingana kama sahani na kawa.

13. Kutoelewana kama maji na mafuta.

14. Kutumika pamoja kama viatu na soksi.

15. Vitu hivyo vinakaribiana kama pua na mdomo.

16. Nyumbani kwao kunakaribiana kama jicho na kope.

17. Mambo yao ni kinyume kama tumbo na mgongo.

18. Ndugu hao wanashirikiana kufanya kazi kama jembe na mpini, kinu na mchi.

 

19. Tunasaidiana kutekeleza jambo hilo mithili ya kata na maji.

20. Jirani hao huogopana ja kondoo na mbwa.

21. Tuliwasaka wezi hao mbele na nyuma.

22. Wao hupatana katika kazi mithili ya kufuli na ufunguo.

23. Wachuuzi hao walitazamana kwa hasira kama jicho na kidole.

24. Wapenzi hao huandamana kama mke na mume.

25. Uhusiano wao ni kama ule wa bwana na kitwana.

26. Yao ni maisha ya upweke. Ni sawa na yale ya maiti na kaburi.

27. Walisaidiana kama maiti na jeneza katika msiba ule.

28. Katika safari yao, walivuka mito na maziwa / mabonde na milima / misitu na nyika.

29. Hali yao ya maisha ni tofauti kama moto na barafu.

30. Auladi wale walishinda wakitazamana kama sakafu na dari. • A14 by smashinghub.com & elImu used under CC_BY-SA
 • A1 by graphicleftovers.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • A2 by www.essentialbaby.com.au › & eLimu used under CC_BY-SA
 • A3 by centenaryarchers.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • B11 by clipartfreefor.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • B1 by worldartsme.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • B2 by www.graphene-battery.net & eLimu used under CC_BY-SA
 • B4 by www.123rf.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • B5 by www.jamesleath.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • B6 by e2ua.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • B7 by ch302.cm.utexas.edu & eLimu used under CC_BY-SA
 • B8 by www.easyfreeclipart.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • B9 by www.houzz.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • image-14 by wqad.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • d10 by https://www.pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • d11 by www.wsj.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • d1 by https://www.modernghana.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • d3 by https://www.flickr.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • d4 by locktechsandiego.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • d7 by 19thcenturyartofmourning.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • d8 by www.melbournefuneral.com.au & eLimu used under CC_BY-SA
 • d9 by www.picswallpaper.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • image-19 by https://www.pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • image-20 by https://www.pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.