Matumizi ya 'o-ote'  by  Joab Otieno

6

Ote ni kivumishi cha kutaja jumla au pamoja au kitu kizima bila kugawanya au kutengganisha.

Mfano

Mlo wote au jumba lote. Ina maana kuwa pamoja au jumla au mzima bila kuacha kingine kando.

Mifano katika sentensi

 • Nguo yote ilichafuliwa.
 • Chakula chote kililiwa.
 • Jumba lote lilisafiswa.


O--ote hutumika kuonyesha kati ya vingine au miongoni mwa. Vitu kadhaa wala si vyote. Baadhi tu, bila kuchagua wala kubagua.


MIFANO KATIKA SENTENSI

 • Mwanafunzi yeyote anaitwa na mwalimu.
 • Chochote kiingiacho mjini si haramu.


Vivumishi ote na o--ote huchukua kiambishijina hivyo huchukuana na ngeli husika kwa mwingiliano thabiti.

ZOEZI

 • Fujo ____ za kisiasa hazifai kamwe na zinafaa kuzikwa katika kaburi la sahau.
 • Ukimwi ni uwele mbaya kwa mja _____.
 • Watu wakiishi bila mpaka _____ wa maisha, watakuwa pakashume
 • Ajira _____ kwa watoto hafai.
 • Mitume _____watakuwa na mkutano wao kesho.

 

MAJIBU

 • Zozote
 • Yeyote
 • Wowote
 • Yoyote
 • Wowote

 

Tathmini

•Kazi hii imeandaliwa na margaret Nguli.
•Shule ya msingi ya milimani .
•           Nairobi.
•           Kenya
 

NOMINO AMBATA

Nominoambata huuundwa kwa nomino mbili (majina mawili) ambazo huambatanishwa na kuwa neno mja.aghalabu maneno yanayounganishwa hayana uhusiano wowote kimaana.


Mifano

Askari + kanzu =askarikanzu

mwana+ mkiwa= mwanamkiwa

Mwana+nchi= mwananchi

Mbwa + mwitu=mbwamwitu

Pembe+tatu=pembetatu

kiinua+mgongo=kiinuamgongo

nusu +kipenyo= nusukipenyo

Simba +marara=simbamarara

KUMBUKA ;maana ya neno yaweza kubadilika kabisa nomino mbili zinapoambanishwa.


MIFANO ZAIDI NA MAELEZO YAKE.

simbamarara (a-wa)---fisi mkubwa

Kivunjajungu (a--wa)---mdudu jamii ya panzi

Mjamziti (a-wa)---mwanamke aliyehimili

Mtambaapanya(u -I) mboriti(miti) inayoshikilia paa

Kiamshakinywa (ki-vi)--chakula cha kwanza cha
asubuhi.

Mwanambuzi (a-wa)--mtoto wa mbuzi.

 

ZOEZI.

Tumia neno mwana kuunda nomno ambata kumi.

 

Mfano

Mwana+ sheria=mwanasheria

mwana+mke+mwanamke.

 

Tazama mifano zaidi

 • Mwana jeshi
 • Mwanasheria
 • Mwanaserere
 • Mwanamaji
 • Mwanandondi
 • Mwanadamu
 • Mwanambuzi
 • Mwanamkiwa
 • Mwanahewa