Tanakali

- Tanakali hutumika kuelezea sauti mbalimbali za mambo. 

Mifano:

 

1. Kutulia tulii.


2. Kunyamaza jii.


3. Kucheka kwakwakwa.


4. Kulia kwikwikwi.


5. Kulala fofofo.


6. Kunukia nhh.
7. Kunuka fee/mff mff.
8. Kubweka bwebwebwe.


9. -eupe pepepe.
10. -eusi pi/titititi.
11. Furaha riboribo/furifuri/mpwitompwito.
12. Kupamba kochokocho.


13. Kujaa pomoni.


14. Kumaliza fyu.


15. Kuchapua miguu chapuchapu.
16. Kuregea regerege.
17. Kuloa rovurovu/lovulovu/chepechepe.


18. Kuponea chupuchupu.
19. Kujifunika gubigubi.


20. Kumwagika mwa.

21. Kutiririka tiriri.


22. Kuchuruzika churururu.
23. Kudondoka ndondondo.
24. Kumulika mwaa.


25. Kunyooka twaa.


26. Kuanguka pahali pagumu pu.


27. Kuanguka mchangani tifu.
28. Kuanguka matopeni pwa.
29. Kuanguka majini chubwi.

30. Kuanguka kwa mtu mnene bwata.
31. Kuanguka kwa shilingi (chuma) sakafuni tangi!

32. Kuanguka kwa kitu chepesi kama vile penseli kacha!
33. Kuteleza parrr.


34. Kuvunjika kenyekenye (kuvunjika kabisa).


35. Mchuzi rojorojo.

36. Matatizo tipitipi.
37. Kuchoka tiki.
38. Kusaga tikitiki.
39. Kubingirika bingiribingiri.


40. Kudunda dududu.
41. Kufunga ndindindi.


42. Kukataa katakata.
43. Kutopata ng’o
44. Kuvurugika vuruguvurugu.
45. Kuteketea teketeke.


46. Kukumbatiana papatu papatu.


47. Kupukutika kupukupu.
48. Kupiga po!
49. Kulewa ndi/chopi/chakari.


50. Huzuni mpwitompwito.

Nukuu sauti zifuatazo

Tumia maneno kwenye mabano.

(chapuchapu, wa, chupuchupu, gubigubi, ndondondo, regerege, mpwitompwito, pomoni, bwebwebwe, fyu)

1. Kubweka ______. 

2. Furaha ______. 

3. Kujaa ______. 

4. Kumaliza ______. 

5. Kuchapua miguu ______. 

6. Kuregea ______. 

7. Kuponea ______. 

8. Kujifunika ______. 

9. Kumwagika _____. 

10. Kudondoka ______. • image-2 by https://pikkiestoolbox.wordpress.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t10 by clipartfreefor.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t11 by ciumpy1923.blogspot.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t12 by www.gingersoftware.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t1 by viralkenya.co.ke › Education & eLimu used under CC_BY-SA
 • t3 by www.clipartbest.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t4 by tuko.co.ke › Crime & eLimu used under CC_BY-SA
 • t5 by atlantablackstar.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t6 by www.globalinfoking.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t7 by https://www.pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t8 by www.brimfulcuriosities.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t9 by https://play.google.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • M1 by https://www.roblox.com/games/140728453/Fall-Down-Stairs used under CC_BY-SA
 • M4 by classified-blog.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • M5 by www.freeimages.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • M6 by www.knuj.net › Recipe Show & eLimu used under CC_BY-SA
 • t13 by https://en.wikipedia.org/wiki/Light & eLimu used under CC_BY-SA
 • t14 by faucetsandfixturespa.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t15 by https://www.pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • M20 by www.democraticunderground.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • M7 by www.waterwarcrimes.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • M89 by https://en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • M8 by https://www.pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • M9 by www.pugetsoundoff.org/blog/ & eLimu used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.