Heshima na adabu

Lugha ya heshima na adabu

- Lugha ya heshima hutumika kutajia mtu na hata mahali mbalimbali.

- Ni vizuri unapoongea na watu utumie maneno ya heshima la sivyo hata nawe hutaheshimiwa.

 

 • Siti: Jina la heshima la mwanamke. Hutumika kabla ya jina lake.
 • Bwana: Jina la heshima kwa mwanamume.
 • Bibi: Jina la heshima kwa mwanamke.
 • Nana: Jina la heshima ambalo hutumiwa kumwitia mwanamke.
 • Mwinyi: Jina la heshima ambalo hutumiwa kumwitia mwanamume.
 • Muadhama: Neno la heshima la kumwitia mtu maarufu (mheshimiwa)

 • Kibibi: Tamko la kumwita mtoto mwanamke.
 • Hayati: Marehemu:

Majina ya heshima ya kumtajia mtu

Mwendazake: aliyeaga dunia

Maneno ya heshima ya kuitikia

Abe hutumika na wanawake kuitikia wanapoitwa.

Bee, Beka, Naam: Neno la kuitikia kwa heshima.

Maneno ya adabu na unyenyekevu

 •  Tafadhali: Neno la heshima la kumwomba mtu afanye jambo kwa  niaba yako.
 •  Shikamoo: Salamu ya heshima itolewayo kwa mtu aliyekuzidi umri.
 •  Samahani: Neno la kuombea msamaha. Neno la kuomba upewe nafasi  au usikilizwe.
 •  Asante: Neno la kuonyesha shukrani kwa yale uliyotendewa.
 •  Ninasikitika:Neno la kuonyeshea hisia za huruma au kuionea hali ya  mtu huruma.
 •  Simile: Neno la adabu la kuomba kupishwa njia.
 •  Ashakum: Neno la kuombea msamha kabla ya kusema jambo  unalofikiria linaweza kumwudhi mtu anayekusikiliza.
 •  Mjamzito: Mwanamke aliyebeba mimba.
 •  Kujifungua:Kupata mtoto.
 •  Msalani/pembeni:Pahali pa kwendea haja.
 •  Pole: Neno la kumwonea mtu huruma au kumsikitikia kutokana na hali mbaya k.v. ugonjwa, kuumia n.k.