Kuandika wingi wa sentensi by
Lilian Luka
6
Tazama picha zifuatazo






Tunaenda kuunda sentensi tukitumia picha tulizoziona.

Samaki wamevuliwa.

Sahani imepangwa sakafuni.

Sahani zimepangwa sakafuni.

Andika sentensi ifuatayo kwa wingi.

Marashi haya ni yangu.

Marashi haya ni yetu.
Andika sentensi zifuatazo kwa wingi
- Wingu limetanda mlimani.
- Uta umewekwa ukutani.
- Mwezi huu umeisha.
Majibu
- Mawingu yametanda milimani.
- Nyuta zimewekwa ukutani.
- Miezi hii imeisha.