Viashiria na viulizi pamoja na ngeli  by   

Viashiria ni nini?

Viashiria ni kivumishi kinachotumiwa kuonyesha kwa kutegemea mahali kulipo kitu kinachoonyeshwa aidha huitwa kionyeshi.

Aina ya viashiria

 • Kiashiria cha karibu - HAPA
 • Kiashiria cha mbali kidogo - HAPO
 • Kiashiria cha mbali sana - PALE

MIFANO KATIKA SENTENSI

 • Mbuzi huyu ni mnono kuliko yule.
 • Mbuzi hawa ni wanono kuliko wale.
 • Kiu chako hicho si kama chake.
 • Embe lile linafanana na hilo.
 • Maembe yale yanafanana na hayo.

ZOEZI

 • Giza ____ (hilo,hiyo,hicho,huo) lilitutisha,
 • Nitakupa vifaa ____ (zako, vyako,yako, chako) sasa hivi.
 • uji ____ (yake, wake, lake, zake) umemwagika.
 • Amechukua kuni ____ (yake, zake, chake, kwake) akaenda
 • Nyumbani ____ (zile, yale,pale,ile) hupendeza.
 • kusafiri ____ (yake, wake, zake, kwake) kulimfurahisha.

MAJIBU

 • HILO
 • VYAKO
 • WAKE
 • ZAKE
 • PALE,
 • KWAKE