Nomino ambata  by  Margaret Nguli

6

Nomino ambata huuundwa kwa nomino mbili (majina mawili) ambazo huambatanishwa na kuwa neno mja. Aghalabu maneno yanayounganishwa hayana uhusiano wowote kimaana.

Mifano

 • Askari + kanzu = askarikanzu
 • mwana + mkiwa = mwanamkiwa
 • Mwana +nchi = mwananchi
 • Mbwa + mwitu = mbwamwitu
 • Pembe + tatu = pembetatu
 • Kiinua + mgongo = kiinuamgongo
 • Nusu + kipenyo = nusukipenyo
 • Simba + marara = simbamarara

KUMBUKA ;maana ya neno yaweza kubadilika kabisa nomino mbili zinapoambanishwa.

MIFANO ZAIDI NA MAELEZO YAKE.

 • Simbamarara (a-wa) ____ fisi mkubwa.
 • Kivunjajungu (a-wa) ____ mdudu jamii ya panzi.
 • Mjamziti  (a-wa) ____ mwanamke aliyehimili.
 • Mtambaapanya(u -I) ____ mboriti (miti) inayoshikilia paa.
 • Kiamshakinywa (ki-vi) ____ chakula cha kwanza cha asubuhi.
 • Mwanambuzi (a-wa) ____ mtoto wa mbuzi.

ZOEZI

Tumia neno mwana kuunda nomIno ambata kumi.

Mfano
 • Mwana+ sheria = mwanasheria
 • mwana + mke = mwanamke

Tazama mifano zaidi

 • Mwana jeshi
 • Mwanasheria
 • Mwanaserere
 • Mwanamaji
 • Mwanandondi
 • Mwanadamu
 • Mwanambuzi
 • Mwanamkiwa
 • Mwanahewa