Maswahili kadirifu

Jibu maswali yafuatayo vilivyo. tumia haya:

adhuhuri, alasiri, machwa, mapambazuko, alfajiri kuu, usiku wa manane, jogoo la kwanza, alfajiri mbichi, utosini, mafungulia ng'ombe, asubuhi, kusi, mafunguliang'ombe, kikupwe, mawanga, machweo, ukame, masika, jogoo la pili, vuli, jioni.

 

1. Msimu wa mvua nyingi huitwa _____.

2. Kishuka huliwa wakati wa_____.

3. Kiporo huliwa lini?_____.

4. Jua huchwa lini?_____.

5. Saa sita usiku ni sawa na _____.

6. Mifugo hurudishwa zizi  kutoka malishoni lini? _____. 

7. Mwendo wa saa tatu hadi saa nne asubuhi ni _____.

8. Machweo ni sawa na ______.

9. Saa nane usiku huitwa _____. 

10. _____ huanzia saa saba hadi saa tisa usiku ilhali _____ huanzia saa kumi hadi saa kumi na moja asubuhi.

 

11. Wakati wa jua la mtikati pia huitwa wakati wa jua la _____.

12. Wakati wa jua linapoaga miti ni sawa na _____.

13. Msimu wa mvua ndogondogo mchoo, vuli au _____.

14. Kwa kawaida gharika hupatikana msimu upi_____.

15. Saa kumi usiku ni sawa na _____.

16. Saa nane mchana hadi magharibi ni ____.

17. Msimu wa baridi kali ni _____.

18. Majira ya kiangazi huitwa _____.

19. Kipindi upepo unapovuma kutokea kusini huitwa ______.

20. Chajio huliwa wakati upi?____

 

Jibu maswali yafuatayo. Jaza jedwali lifuatalo

 Siku                                           Tarehe

1. Ijumaa                                 Septemba ishirini           Jana

2. Jumamosi

3.

4.

5.

6.

7.

8. Iwapo juzi ilikuwa siku ya jumatatu, je, leo ni siku ipi?

9. Juma ataenda kumwona shangazi siku ya nne kuanzia leo. Kwa hivyo ataenda siku ya _____.

10. Mtondo hutanguliwa na _____.

11. Usiku wa kuamkia siku fulani huitwa _____.

12. Mwanzoni mwa mwaka ni _____.
13. Nilitoka kwetu siku ya ijumaa na nikarudi siku tatu baadaye. Je, nilirudi siku ipi?

14. Kesho ya kesho ni _____.

15. Juzi hufuatwa na _____.