Vimelea

- Vimelea ni mimea au wadudu wanaoishi kwa kuvitegemea viumbe au mimea mingine.

- Katika binadamu, tuna vimelea wa nje na wengine hukaa ndani ya mwili wa binadamu.

Mifano ya vimelea wa nje:

1. Kiroboto – mdudu aumaye, hukaa mavazini au manyoyani.

2. Kitumbi – funza apenyaye ngozi ya mtu na kukaa huko.

3. Chawa – mdudu akaaye mwilini mwa mwanadamu, nguo chafu na nywele chafu.

4. Kunguni – mdudu afyonzaye damu na hukaa vitandani, pongoni, vitini n.k.

5. Funza/tekenya/bombwe – mdudu akaaye kwenye miguu ya watu.

6. Mbung’o/ndorobo/chafuo/pange– mdudu kama nzi na aumaye na kusababisha malale.

7. Mbu – mdudu afyonzaye damu na kusababisha malaria.

8. Papasi – mdudu mweupe afananaye na kunguni na huuma. Huleta homa ya vipindi kwa binadamu.

 Zoezi: Jibu maswali yafuatayo kikamilifu.

1. Kimelea kinachoishi kwenye nywele chafu ni ____________.

2. Kimelea cha ndani kinachoishi tumboni ____________.

3. Kimelea kinachosababisha uele wa malale ni ____________.

4. Kimelea ambacho kikikua huwa funza ni

5. Kimelea kinachosababisha homa ya muda kwa binadamu ni ____________.

6. Kimelea kipendacho kujificha kitandani na hunyonya damu wakati mtu amelala ni ____________.

7. Kimelea kipendacho kunata ngozini mwa mbwa na wanyama wengine ni ____________.

8. Kimelea kinachosababisha ugonjwa wa malaria ni ____________.