Vimelea

 

- Vimelea ni mimea au wadudu wanaoishi kwa kuvitegemea viumbe au mimea mingine.

- Tafsiri ya vimelea kwa kiingereza ni 'Parasites'.

- Katika binadamu, tuna vimelea wa nje na wengine hukaa ndani ya mwili wa binadamu. 

- Inamaanisha kuwa kuna vimelea wanaoathiri wanadamu na wale wanaoathiri wanyama. 

Mifano ya vimelea wa nje:

1. Kiroboto – mdudu aumaye, hukaa mavazini au manyoyani.

2. Kitumbi – funza apenyaye ngozi ya mtu na kukaa huko.

3. Chawa – mdudu akaaye mwilini mwa mwanadamu, nguo chafu na nywele chafu.

4. Kunguni – mdudu afyonzaye damu na hukaa vitandani, pongoni, vitini n.k.

5. Funza/tekenya/bombwe – mdudu akaaye kwenye miguu ya watu.

6. Mbung’o/ndorobo/chafuo/pange– mdudu kama nzi na aumaye na kusababisha malale.

7. Mbu – mdudu afyonzaye damu na kusababisha malaria.

8. Papasi – mdudu mweupe afananaye na kunguni na huuma. Huleta homa ya vipindi kwa binadamu.