Utangulizi

- Mnyama ni kiumbe ambacho kina uhai wala sio mtu, mdudu au mmea.

- Kuna wanyama wanaokaa nyumbani (mifugo).

- Wanaoishi kichakani (wanyamapori).

- Mifugo huwekwa kwa minajili ya pato kwa binadamu. Wanyamapori pia ni kivutio kikubwa sana kwa watalii.

- Kwa hivyo basi, wanyama wote wanastahili kutunzwa na kuhifadhiwa vilivyo.