Maswali kadirifu

Jaza mapengo katika sentensi zifuatavyo

 

1. Mchezo wa kushikana na kuangushana huitwa _____.

2. Jina jingine la mchezo wa soka ni mchezo wa _____.

3. Mchezo wa ngumi pia huitwa _____.

4. Mchezo wa soka huwa na wachezaji wangapi kila upande?

5. Mchezo wa kuruka kwa kutumia mti huitwa?

6. Mchezo wa watoto wa kugotanisha miguu miwili pamoja na kurukaruka kwa kwenda mbele na nyuma ni _____.

7. Mchezo wa kuvuta kamba wa timu za watu kumi na wawili kila upande huitwa _____.

8. Mashindano ya mbio za farasi au watu ni _____.

9. Mchezo wa magongo uchezwao na watu wawili au wanne ambao huingiza mipira katika vishimo huitwa _____.

10. Mbio za vijigari vidogo huitwaje?

 

Toa maelezo kuhusu michezo ifuatayo.

 • mwajificho
 • gofu
 • gozi
 • riadha
 • tenisi
 • bao
 • kibunzi
 • sataranji
 • gungwi
 • kibafute
 • netiboli
 • mpira wa vikapu
 • jugwe
 • raga
 • mpira wa magongo
 • miereka
 • judo
 • urushaji sagai
 • kuruka kwa upondo
 • mpira wa vinyoya