Maswali kadirifu

A. Teua jibu lifaalo ili kujaza kila pengo

kilindi   zilizala   kifungulima  kisiwa  kisulisuli  ufuo  tambarare  ziwa  chemchemi   unyevu   ukungu  mwambao  ghuba   bonde  barafu

1.  _____ ni hali ya kuwa majimaji.

2. _____ ni jiwe lipatikanalo baada ya maji kuganda kwa baridi.

3. Moshi mweupe utandso angani huitwa _____.

4. Sehemu iliyo na maji na iliyozungukwa na nchi kavu huitwa _____.

5. Tao la pwani huitwaje?_____.

6. Sehemu ya ardhi au nchi kavu iliyo baina ya vilima huitwaje ____.

7. Ukingo wa bahari huitwa ____.

8. Sehemu ya nchi isiyokuwa na mwinuko wala mbonyeko huitwa ____.

9. Mahali ambapo maji hububujika huitwa _____.

10. Tetemeko la ardhi pia huitwa _____.

11. Sehemu iliyo karibu na pwani huitwa _____.

12. _____ ni upepo mkali unaoenda kwa mizunguko.

13. Nchi kavu iliyozungukwa pande zote na maki huitwa _____.

14. _____ ni kisima cha jangwani.

15. Bandari iliyojaa maji mengi huitwa _____.

 

B. Toa maelezo kuhusu maneno yafuatayo.

  1. mazingira mto
  2. bahari
  3. ziwa
  4. kilele
  5. mwangwi
  6. genge
  7. madini
  8. bonde la ufa
  9. rasi

C. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo

Nchi ya Kenya inasifika kote duniani kutokana na hali nzuri ya hewa. Nchi hii hupatikana katika ukanda wa Ikweta. Jua hupatikana kwa mwaka mzima. Hali hii nzuri ya hewa huwavutia watalii chungu nzima kutoka kila pembe ya dunia. La kushangaza ni kuwa, hali ya hewa hutofautiana sana kutoka sehemu moja ya nchi hadi nyingine. Ukienda nyanja za juu na maeneo ya milima kama vile mlima Kenya, utapata hali ya baridi. Kileleni mwa mlima Kenya kuna hata theluji. Uteremkapo kuelekea Mwambao wa Pwani, viwango vya joto huwa juu kutokana na bahari Hindi. Maeneo ya ziwa Viktoria pia hupata viwango vya juu vya joto.

Mbali na hali nzuri ya hewa, ipo misitu iliyojaa wanyama pori wa kila aina na miti ya kila aina. Kadhalika kuna mbuga na hifadhi za wanyama. Hili huwa ni vutio kubwa kwa watalii. Aidha, kuna mito iliyo na mianguko ya maji. Mfano mzuri ni mwanguko wa Thompson na mianguko ya Thika na Chania. Kunazo chemchemi za maji moto katika Bonde la Ufa ambazo huwaacha watalii vinywa wazi. Isisahaulike kuwa ni katika mkoa uo huo wa Mwanya Mkuu ambapo ipo milima ya ajabu kama vile Menengai ambao una kreta kileleni. Kutokana na mvua ya kutosha, mazao mengi hukuzwa katika sehemu nyingi za nchi. Mimea hiyo ni kama vile, miwa, mibuni, mipareto, mpunga, mipamba, michai, mikademia nikitaja tu michache. Yapo pia madini kama vile magadi huko Magadi, chokaa n.k. Je, wajua nchi hii ina misimu minne katika mwaka?

 

Jibu maswali yafuatayo

1. Taja maliasili yaliyotajwa katika kifungu hiki?

2. Taja malighafi yaliyotajwa katika kifungu.

3. Taja bidhaa zipatikanazo kutokana na malighafi hayo.

4. Taja mbuga nne za wanyama pori nchini Kenya.

5. Taja hifadhi nne za wanyama nchini Kenya.

D. Jibu maswali yafuatayo.

1. Madini yatumikayo kukatia vioo huitwa ______________.

2. Madini yatumiwayo kutengenezea mapambo ya fahari k.v. pete huitwa ______________.

3. Madini magumu yatumiwayo kukata vyuma huitwa ______________.

4. Madini majimaji yenye rangi ya fedha yatumiwayo katika themometa huitwa?

5. Madini meupe yatumiwayo sana kupaka juu ya chuma kuzuia kutu? 6. Madini ya chumvi chungu yatumiwayo kutengenezea sabuni ni ______________.

7. Unga mweupe upakwao kuta za nyumba ni ______________. 8. Madini ya rangi nyekundu yanayong’aa baada ya kusuguliwa na hutengenezea nyaya za umeme ni ______________.

9. Madini meupe yachimbwayo ardhini na hutumika kutengenezea vioo na ng’amba za sanaa ni ______________.

10. Madini ya buluu na kijivu hafifu ambayo huyeyuka rahisi ikichomwa ni ______________.

E. Jibu maswali yafuatayo.

1. Madini yatumikayo kukatia vioo huitwa ____.

2. Madini yatumiwayo kutengenezea mapambo ya fahari k.v pete huitwa _____.

3. Madini magumu yatumiwayo kukata vyuma huitwa _____.

4. Madini majimaji yenye rangi ya fedha yatumiwayo katika themometa huitwa?

5. Madini meupe yatumiwayo sana kupaka juu ya chuma kuzuia kutu?

6. Madini ya chumvi chungu yatumiwayo kutengenezea sabuni ni ____.

7. Unga mweupe upakwao kuta za nyumba ni _____.

8. Madini ya rangi nyekundu yanayong'aa baada ya kusuguliwa na hutengenezea nyaya za stima  _____.

9. Madini meupe yachimbwayo ardhini na hutumika kutengenezea vioo na ng'amba za sanaa ni _____.

10. Madini ya buluu na kijivu hafifu ambayo huyeyuka rahisi ikichomwa ni _____.

Zoezi F

  1. Taja madini matano yaitwayo vito.
  2. Taja madini yatumiwayo viwandani kuyeyushia vyuma.
  3. Madini yapi yaliyovumbuliwa hivi karibuni nchini Kenya katika Kaunti ya Kwale?
  4. Ni madini gani yatengenezwayo kalamu?
  5. Mhunzi hutumia madini yapi?
  6. Sonara upenda kutumia madini yapi ?
  7. Taja madini giligili au maowevu.
  8. Taja madini yanayotengeneza mabamba.
  9. Madini yapi yanayotengenezwa sarafu?
  10. Madini yapi yanayofuliwa mapambo kama vile: vidani, bali na pete?
  11. Madini yapi ni kiungo cha kitoweo?
  12. Taja madini yanayotumiwa na mjumu.
  13. Taja madini yanayotumika kutia nakshi kuta za nyumba.