Maswali kadirifu

A. Taja majina ya vikembe vya viumbe vifuatavyo

  • bakari -
  • nyuni -
  • simba -
  • sungura -
  • papaupanga -
  • kuku -
  • mnyau/paka -
  • farasi na punda -
  • samaki -
  • njiwa -
  • dagaa -
  • mbwa -
  • chungu -
  • suria - 
  • kipepeo -
  • nyuki -
  • nzi -
  • mbu -
  • chura -

B. Jibu maswali yafuatayo.

  1.   Kitungule ni kikembe cha ______ naye shubli ni kikembe cha _______.
  2.   Mtoto wa mbuzi ni ______ naye wa kondoo ni _______.
  3.   Mwana wa papa ni _____ naye wa nyangumi ni ______
  4.   Mtoto wa nzi ni ______ naye wa nyuki ni _______.
  5.   Ndama ni mtoto wa ________ pia mwana wa ndovu huitwa _______.
  6.   Mwana wa punda ni _______ naye wa paka ni ______.
  7.   Kivinimbi ni mtoto wa ______ naye kingonyo ni mtoto wa ________.
  8.   Mwana wa chura ni _____ na yule wa kipepeo ni ________.
  9.   Mwana wa mbu ni _____ naye mwana wa nyoka ni ______.
  10.   Mwana wa chui ni ______ na yule wa mdudu ni _______.