Semi na nahau

Nahau ni maneno yenye maana maalum ambayo hayajatokana na maana za kawaida za maneno hayo.

Zifuatazo ni nahau za kuelezea hali mbalimbali

 • kuoa – kupata jiko, kuasi ukapera, kufunga ndoa/nikahi/nikaha, kufunga pingu za maisha.

 • kufanya bidii – kujifunga nira, kujifunga masombo, kujifunga kibwebwe.

 

 • kufa – kwenda jongomeo, kwenda kuzimuni, kufuata njia ya marahaba, kupungia dunia mkono wa buriani, kutangulia mbele ya haki, kuipa dunia kisogo, kukata kamba, koma moyo
 • kuwa mzembe – kulaza damu, kuwa kupe, kuwa chaza, kuwa na mkono mzito.

 • kupona – kupata nafuu, kuona ashekari, kuona afueni.
 • kuwa na bahati – kuwa na ndege mzuri, kushukiwa na nyota ya jaha, kuwa na mkono mzuri

 

 • kuvumilia matatizo – kuuma meno, kumeza mate machungu.

 • kufukuzwa kazini – kupigwa kalamu, kuonyeshwa mlango, kuonyeshwa paa, kumwaga unga.

 

 • kuharibika kwa jambo au mambo – mambo kwenda mrama, mambo kwenda shoto, mambo kwenda upogo, mambo kwenda segemnege, mambo kutumbukia nyongo.

 • kupuuza – kutemea mate, kuonyesha mgongo, kuvalia miwani, kufumbia macho.
 • kuongea maneno ya busara – kutoa lulu.
 • kuongea maneno yasiyo na maana – kutoa ngebe, kutoa maneno ya mkahawani.

 

 • kudanganya – kutia kiwi, kupaka mafuta kwa tako au kwa mgongo wa chupa, kumpatia mtu ulimi wa kulazia, kupiga mafamba, kuuza upepo kwa dunia, 
 • kucheza kayaya za chini kwa chini -  kujuta – kuuma vidole

 • kukimbia hatari – kuchana mbuga, kutimua mbio, kutoka shoti, kusema mguu niponye, kuponda wa fisi, kutwika miguu mabegani.
 • kutembea – kupiga miguu, kupiga milundi.
 • kulewa pombe – kupiga maji, kuvaa miwani, kuchapa mtindi.

 

 • kukasirika – kupandwa na mori, kupandwa na mafutu, kuchemkwa na damu, kuchemkwa na nyongo, kupandwa na madadi. 

 • kufikiria sana – kujikuna kichwa.

 • kupatwa na matatizo – kupigwa na urumo, kula mumbi, kuogelea kwenye mchanga wa moto, kuingia kwenye maji makuu, maji kuwa ya shingoni, kuingia kwenye tanuri la moto, maji kuzidi unga.
 • kuwa na tamaa – kuwa na mate ya fisi, kumezea kitu mate
 • kuomba kwa Mola – kupiga dua, kupiga bisimillahi

 • kuwa na njaa – kubanwa na kapu.
 • kula chakula – kushtaki njaa, kufanyia mlo/chakula haki.

 • kukamatwa – kutiwa mbaroni, kutiwa nguvuni.
 • kufungwa gerezani – kula kalenda.
 • kuzungumza – kupiga soga, kula gumzo, kula nyama ya ulimi.

 

 • kushinda – kufua dafu

 • kupoteza matumaini – kufa moyo, kuvunjika moyo, kukata tamaa.
 • kupotea njia – kukanyaga chechele

 

 • kutoa rushwa – kuzunguka mbuyu, kupiga konde la nyuma, kutoa mlungula.
 • kupata upinzani – kutolewa jasho,
 • kutolewa kamasi - kukonda, kuwa fremu, kuwa gofu,

 

 • kukaukwa na damu, - kuwa mfupa.
 • kumkanya mtu – kumshika sikio.
 • kumpa mtu pole – kumpa mkono wa tanzia.

 • kuwa mchoyo – kuwa na mkono wa birika/buli, kuwa joka la mdimu.
 • kuongoza – kushika usukani, kushika hatamu za uongozi.

 • kuondoka – kung’oa nanga.

 

 • kuwa wa mwisho – kushika mkia, kushika nanga.
 • kufikia mwisho – kutia nanga, kufikia ukingoni.
 • kufitini – kutia fitina, kutia chuku, kutia utambi, kuchoma nguru.

 • kumaliza kiu ya maji – kukata kiu, kukonga roho.
 • kumwomba mtu msamaha – kumwangukia mguuni.

 • kumheshimu mtu – kumvulia kofia, kumshika miguu.

 

 • kufanya kazi – kuzimbua riziki, kutafuta unga, kushika mpini, kumwaga jasho.
 • kumwaibisha mtu -kumvunjia mtu mbeleko, kumvua mtu nguo. kumpaka mtu mavi, kumpaka mtu vumbi.
 • kumtia kiraka - kuwa adui, kutopaliana moto, kutopikika katika chungu kimoja, kuwa maji na mafuta. • kuoa by www.weddingbycolor.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t1_3 by riosuerte.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t2_3 by https://en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • kuwa_na_bahati by www.hapakenya.com & eLimu used under CC_BY-ND
 • t3_3 by www.distance-education.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • t4_3 by www.clipartpanda.com/categories/depressed-girl-clipart & eLimu used under CC_BY-SA
 • 5cdca5a3-a516-418c-9845-edab0b3a743b by http://www.daily-mail.co.zm/can-date-drunkard/ used under CC_BY-SA
 • kukasirika by https://www.pinterest.com/HappySurprise/angry-birds/ & eLimu used under CC_BY-SA
 • kuomba_kwa_Mola by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • t6_1 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • kushinda by www.kenyapage.net & eLimu used under CC_BY-SA
 • kuzungumza by https://citizentv.co.ke & eLimu used under CC_BY-SA
 • image-12 by offoindia.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • kumpa_mtu_pole by https://www.illustrationsource.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • 78 by https://matatumedia.wordpress.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • kuongoza by www.forbes.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • image-16 by www.stormfront.org & eLimu used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.