Methali

- Methali hutumika kwa njia mbalimbali.

- Methali hutumika kwa;

 • ushauri
 • maonyo
 • kutoa motisha n.k.

Yasome kwa makini makundi yafuatayo ya methali.

Methali zinazotuonya kutoringa tunapofanikiwa

                

 • Pavumapo palilie si kazi kudamirika.       
 • Ajidhaniye amesimama aangalie asianguke.
 • Mpanda ngazi hushuka.

 • Aliye juu mngoje chini.    
 • Usione kwenda mbele kurudi nyuma si mkazi.
 • yakijaa hupwa.

Methali zinazohimiza ushirikiano 

 • Jifya moja haliinjiki chungu.

 • Mkono mmoja hauchinji ng’ombe.

 • Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
 • Mkono mmoja haulei mwana.
 • Ukuni mmoja hauwaki jikoni.

 • Mkataa wengi ni mchawi.

Methali zinazotuonya kutodanganyika na uzuri wa nje               

 • Yote yang’aayo si dhahabu.

 • Vyote viowevu si maji.
 • Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
 • Penye urembo ndipo penye ulimbo.

 • Uzuri wa kuyu ndani mabuu.  

Sihadaike na rangi, tamu ya chai si sukari.

Methali zinazo himiza kuwa na bidii.

 • Mtaka cha mvunguni sharti aina

Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.

 • Achanikaye kwenye mpini wa jembe hafi njaa.

 • Atangaye sana na jua hujua.      

 • Kwenda bure si kukaa bure.                                          
 • Mchuma juani hula kivulini.  

 • Ukiona vyaelea vimeundwa.      
 • Kilicho baharini kakingoje pwani.      

          

 • Bahati ni chudi.        
 • Ajizi nyumba ya njaa.    

 • Zohali ni nyumba ya njaa
 • Mwana mtukutu hali ugali mtupu.

Methali zinazohimiza uvumilivu

 • Umemla ng’ombe mzima usishindwe na mkia.
 • Mvumilivu hula mbivu.

Kenda i karibu na kumi.       

 • Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
 • Zito hufuatwa na jepesi.
 • Penye nia pana njia.  

         

 • Baada ya dhiki faraja.


 • Penye mawimbi na milango i hapo.
 • Tone kwa tone huwa mchirizi.      
 • Tembe kwa tembe huwa mkate.

Methali zinazotuonya kuhusiana na tamaa

 • Mtaka yote hukosa yote.
 • Tamaa mbele mauti nyuma.

 • Njia mbili zilimshinda fisi.
 • Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
 • Mla kwa miwili hana mwisho mwema.
 • Tamaa ilimwua fisi.

 • Haraka haraka haina baraka.
 • Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
 • Mwenye pupa hadiriki kula tamu.

Methali za kutuonya kutocheka hali za wengine.

 • Nyani hucheka wengine ngoko.
 • Ajabu ya kipofu kumcheka chongo.
 • Nyani haoni kundule.

 • Ajabu ya kibogoyo kumcheka mapengo.
 • Ajabu ya ngamia kucheka nundu ya ng’ombe.

Methali zinazotushauri kuuthamini uhusiano wa kidamu

 •  Ndugu ni kufaana si kufanana.

 • Damu ni nzito kuliko maji.
 • Ndugu mui heri kuwa naye.
 • Isipowasha hunzaye.
 • Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
 • Damu ni damu si kitarasa.
 • Zimwi likujualo halikuli likakwisha

Methali zinazotushauri tuyashughulikie matatizo mapema

1. Udongo uwahi ungali maji.

2. Kambare mkunje angali mbichi.

3. Chuma kiwahi kingali moto.

4. Upatilize udongo ungali maji.

5. Usipoziba ufa utajenga ukuta.

Methali zinazotuhimiza kutenda mema

 •  Kwendako mema hurudi mema.
 •  Jaza ya ihsani ni ihsani.
 •  Tenda wema uende zako.
 •  Wema hauozi.
 •  Kumpa mwenzio si kutupa.

Methali za kutueleza kutokuwa na matumaini makubwa kabla jambo halijatimia

 •  Usikate kanzu kabla mwana hajazaliwa.
 • Usihesabu vifaranga kabla hawajaanguliwa.

 • Kutangulia si kufika.
 •  Kuchumbia si kuoa.
 • Kulenga si kufuma.

Methali zinazotuonya kutotegemea usaidizi ulio mbali

 •  Kamba ya mbali haifungi kuni.
 •  Akiba kibindoni silaha iliyo mkononi.
 •  Ulingo wa Kwae haulindi Manda.
 •  Fimbo ya mbali haiui nyoka.
 • Sanda ya mbali haiziki maiti.

Methali za kuonyesha hali ya kukata tamaa.

 • Cha kuzama hakina nahodha.

 •  Sikio la kufa halisikii dawa.
 • Cha kuoza hakina ubani.
 • Cha kuanguka hakina rubani.

Methali zinazoeleza mabadiliko maishani

 •  Dunia ni rangi rangile.
 •  Dunia ni mwendo wa ngisi.
 •  Dunia ni duara huzunguka kama pia.
 •  Dunia ni mti mkavu kiumbe usiuegemee.
 •  Dunia ni tambara bovu.

Methali zinazotuliwaza na kutuonyeshauwezo wake Muumba

 •  Jitihada haiondoi kudura.
 •  Jitihada haiondoi amri ya Mungu.
 •  Yakija yapokee.
 •  Usibishane na shani ya Mungu.
 •  Kalamu ya Mungu haikosi.
 •  Liandikwalo halifutiki.

Methali za kuwaliwaza wanyonge

 •  Mnyonge hana haki.
 •  Ng’ombe wa mkata hazai jike.

 • Dau la mnyonge haliendi joshi.

 •  Mnyonge kupata ni mwenye nguvu kupenda.

 •  Fimbo ya mnyonge hulipwa na Mungu.
 •  Mhini na mhiniwa njia yao ni sawa (moja).
 • Cha mfupi huliwa na mrefu
 •  Cha mfupi huliwa kichwani • m1 by orthodoxwayoflife.blogspot.com/2014_04_01_archive.html used under CC_BY-SA
 • m2 by nqobile87.wordpress.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • m3 by newburyportchamber.org/pages/CityInformation used under CC_BY-SA
 • m4 by www.electricconsumer.org/recipes/ham-and-beans/ used under CC_BY-SA
 • m5 by https://www.flickr.com/photos/enjoynizam/6317182239 used under CC_BY-SA
 • m6 by campfirenow.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • d10_1 by actsforaee.blogspot.com/2016/02/facts-poorest-countries-in-world.html & eLimu used under CC_BY-SA
 • d1_1 by www.forumforhinduawakening.org/.../benefit-from-wearing-sattvik-orna... & eLimu used under CC_BY-SA
 • d3_1 by www.polyvore.com/tea_cups/collection?id=2776890 & eLimu used under CC_BY-SA
 • d4_1 by alkasibfoundation.blogspot.com/2012_11_01_archive.html & eLimu used under CC_BY-SA
 • d5_1 by https://en.wikipedia.org/wiki/Vacation_(2015_film) & eLimu used under CC_BY-SA
 • d6_1 by https://kqduane.com/.../longform-essay-why-do-christian-men-work-so-ha... & eLimu used under CC_BY-SA
 • d7_1 by https://en.wikipedia.org/wiki/Sand & eLimu used under CC_BY-SA
 • d8_1 by ee.co.uk/orange & eLimu used under CC_BY-SA
 • d9_1 by www.shore.nsw.edu.au & eLimu used under CC_BY-SA
 • n2 by https://en.wikipedia.org/wiki/Manual_labour & eLimu used under CC_BY-SA
 • n3 by https://plus.google.com/+EdgarFlores1979 & eLimu used under CC_BY-SA
 • n4 by shopping.indiatimes.com › ... › Televisions › LED TVs & eLimu used under CC_BY-SA
 • n7 by https://play.google.com/store/apps/details?id=com.altsoldev...hl=en & eLimu used under CC_BY-SA
 • t1_2 by communicatebetterblog.com/the-waiting-line/ & eLimu used under CC_BY-SA
 • t2_2 by www.slideshare.net/bright9977/acres-of-diamonds-13357070 7 & eLimu used under CC_BY-SA
 • t3_2 by https://www.cars.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • t4_2 by https://www.megapixl.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • a1 by contraindications5.rssing.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • a2_1 by funnyjunk.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • y1_1 by scribol.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • y3_1 by https://www.mydish.com/ used under CC_BY-SA
 • 1 by www.cartoonnetwork.comb & eLimu used under CC_BY-SA
 • 2 by www.cartoonnetwork.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • 3 by www.hha.org.au & eLimu used under CC_BY-SA
 • 4 by slideshare.net & eLimu used under CC_BY-SA
 • 5 by www.wordstream.com/online-advertising & eLimu used under CC_BY-SA
 • 6 by www.cartoonnetwork.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • 7 by www.cartoonnetwork.com/games & eLimu used under CC_BY-SA
 • 8 by www.cartoonnetwork.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • 10 by www.goldenfoundation.biz/index.php used under CC_BY-SA
 • 11 by www.laptop-recycling.com/charity-work.html used under CC_BY-SA
 • 15 by content.time.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • 16 by www.healthychicksandmore.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • 17 by slideplayer.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • 20 by animalsversesanimals.yuku.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • 25 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • 26 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • 27 by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • dunia by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • muumbe by Unknown used under Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License
 • hdhd by kenrich.me/page/121/change-for-children & eLimu used under CC_BY-SA
 • jgjg by huffmansinkenya.blogspot.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • mbm by anzetsewere.wordpress.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • nvnv by jesuschristsymphonyorchestra.blogspot.com & eLimu used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.