Wakati

Wakati

Katika lugha ya Kiswahili tunazo nyakati mbalimbali. Nyakati hizi huwakilishwa kwa viambishi mbalimbali. Nyakati hizi huashiria majira au muda mbalimbali.

  • Wakati uliopo (wakati wa leo) Kiwakilishi – n a – hutumika. k.m: Mtoto anacheza matopeni;

Wanafunzi wanasoma.

  •  Wakati uliopita (wakati wa jana) Kiwakilishi – l i – hutumika k.m. Mtoto alicheza matopeni; Wanafunzi walisoma.
  •  Wakati ujao (wakati wa kesho) Kiwakilishi – t a – hutumika k.m. Mtoto atacheza matopeni;Wanafunzi watasoma.
  •  Wakati wa mazoea (kila wakati) Kiwakilishi – h u – hutumika k.m. Mtoto hucheza matopeni; Wanafunzi husoma. Muhimu Katika wakati wa mazoea, kiwakilishi cha wakati ndicho hutangulia katika kitenzi. Kiwakilishi cha nafsi hakiwekwi kwenye kitenzi k.m. Mtoto husoma kwa bidii.

  •  Wakati uliotimia (timilifu). Wakati wa me. Kiwakilishi me hutumika k.m. Mtoto amecheza matopeni; Wanafunzi wamesoma.
  •  Wakati ujao kuendelea kwa kitendo Wakati huu huonyesha kuwa kitendo kitakuwa kikiendelea wakati ujao. -takuwa na ki– hutumika k.m Mtoto atakuwa akicheza matopeni; Kesho wanafunzi watakuwa wakisoma. Muhimu Ni makosa kutumia –takuwa pamoja na –na–. Mtoto atakuwa anacheza X
  • Wakati uliopita hali ya kuendelea kwakitendo Wakati huu huonyesha kuwa kitendo kilikuwa kikiendelea wakati uliopita. likuwa na –ki– hutumika k.m. Juzi, mtoto alikuwa akicheza matopeni; Jana wanafunzi walikuwa wakisoma. Muhimu Ni makosa kutumia –likuwa pamoja na –na–. Mtoto alikuwa anacheza matopeni. X

  • Wakati uliotimia (timilifu) hali ya kuendelea Huonyesha kitendo ambacho kimekamilika lakini kilikuwa kikiendelea muda mfupi tu uliopita. -likuwa na – m e – hutumika k.m. Mtoto alikuwa amecheza matopeni;

Wanafunzi walikuwa wamesoma.

  •  Wakati uliopita kufuatana kwa vitendo Hutuonyeshea kuwa, vitendo kadhaa vilifanyika kwa kufuatana. –li– hufuatwa na –ka– k.m. Badala ya: Aliamka. Alijitayarisha. Aliondoka. Alisafiri. Alifika. Tutasema: Aliamka, akajitayarisha, akaondoka akasafiri na akafika.

(Katika sentensi hii, tumetumia kiambishi –li– katika kiarifu cha kwanza kisha tukatumia –ka– katika viarifu vilivyofuata).

  •  Wakati ujao kutimia kwa kitendo Mtoto atakuwa amefika.



  • wakati_1 by https://www.pinterest.com/cca0522/sports/ used under CC_BY-SA
  • wakati_2 by whotalking.com/flickr/KCSE & eLimu used under CC_BY-SA
  • Untitled-1 by unknown & eLimu used under CC_BY-SA
  • wakati_1_1 by https://www.pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA
  • wakati_2_1 by whotalking.com/flickr/KCSE & eLimu used under CC_BY-SA

  • Creative Commons License
    All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.