Kiambishi na kirejelei

Kiambishi na kirejelei

Kiambishi na kirejelei hutumika kuonyeshea hali ya kumiliki.

Ili kiambishi na kimiliki vitumike, sharti pawe na angalau nomino mbili nomino iliyomiliki na inayomilikiwa.

Kiambishi huwakilisha nomino miliki nacho kirejelei hurejelea nomino milikiwa.

 

Kiambishi ki kinawakilisha kitabu (nomino miliki) nacho kirejelei yo kinarejelea michoro (nomino milikiwa).

Ili kuelewa mada hii ni sharti uelewe viashiria vya kwanza katika kila ngeli ya nomino miliki na kiwakilishi amba- kwa nomino milikiwa.

Aidha, ni sharti uvielewe viwakilishi vya nafsi zile tatu. 

Kiambishi na kirejelei cha mwisho(Wakati wa mazoea)
Kulingana na nyakati, kirejelei kinaweza
kutumika katikati ya kiarifu au mwishoni
mwa kiarifa.
k.m. Mtoto anayecheza (wakati uliopo).
Mtoto aliyecheza (wakati uliopita).
Mtoto atakayecheza (wakati ujao).
Mtoto achezaye (wakati wa mazoea).

Kiambishi na kirejelei cha mwisho hutegemea mambo mawili:

  • Ngeli ya nomino husika.
  • Mnyambuliko wa kiarifa husika.

Tazama mifano hii

  • Mchezo achezao (kufanya)
  • Mchezo uchezwao (kufanywa)

Katika mfano wa kwanza, kiambishi (a) kinawakilisha mtendaji yaani achezaye ilhali
katika mfano wa pili kiambishi (u) kinawakilisha kitendewa yaani mchezo.

Kirejelei ʻoʼ cha tamati (mwisho)
Kirejelei ‘o’ hutumika mwishoni mwa kiarifu (kitenzi) katika wakati wa mazoea.
Ziangalie sentensi zifuatazo.

  • Mtoto ambaye hujitahidi hufua dafu (kiwakilishi amba-)

Mtoto ajitahidiye hufua dafu. (kirejelei ‘o’)

  • Kitabu ambacho hutumiwa hukikanganyi (kiwakilishi amba)

Kitabu kitumiwacho hakikanganyi. (kirejelei ‘o’)

Kisigino kiumiacho hutibiwa.
1. Wembe ambao hunyolea ni safi.
2. Jino ambalo huuma hung’olewa.
3. Mechi ambayo huchezwa hupendeza.
4. Maswali ambayo huulizwa hujibiwa.
5. Kibandani ambako husafishwa huvutia.
6. Mwanafunzi ambaye hujitahidi hufua
dafu.
7. Kazi ambazo hufanywa kwa makini
huvutia.
8. Watu ambao hushirikiana hupiga hatua.
9. Kuiga ambako hupotosha hakufai.
10. Nyumbani ambapo hupiganwa hapafai.
11. Maumbo ambayo huchorwa yanafaa
12. Darasani ambamo hupanguzwa ni mwa
mwalimu
13. Ugonjwa ambao huenezwa ni hatari.
14. Jani ambalo huanguka ni kavu.
15. Hali ambayo huzungumsiwa ni nyeti.

-enye na ʻoʼ rejeshi
Tayari tumeona kuwa kivumishi – enye hutumika kuonyeshea hali ya kumiliki. Aidha
‘ o’ rejeshi vilevile inaweza kutumika kuonyeshea hali ya kumiliki.
Iangalie mifano ifuatayo:

  • Mtoto mwenye pipi mkononi.
  • Mtoto aliye na pipi mkononi.

 

A-unganifu
A-unganifu hutumika kuonyeshea uhusiano kati ya nomino mbili au vitenzi. A-unganifu hubadilika kutoka ngeli moja hadi nyingine.
Tazama jedwali lifuatalo: