Aina na za nomino

Kwa jumla, tuna aina nne kuu za nomino:

1. Nomino za viumbe vilivyo na uhai na roho

Mifano

watu, wanyama, wadudu, vimelea vya wanyama (k.v. kupe, chango n.k.)

2. Nomino za vitu visivyo na uhai (isipokuwa mimea)

Mifano

meza, darasa, kijiko, gari, nyimbo, chakula, vinywaji n.k.

3. Nomino za mahali

Nomino hizi hupatikana tuongezapo silabi “ni” mwishoni mwa baadhi ya nomino za vitu k.m. meza – mezani; darasa – darasani, mguu – mguuni n.k

4. Nomino za dhahania/ nadharia (za kuelezea hali)

Mifano

woga, ufanisi, wembamba, werevu, wema, utiifu n.k. Aina hizi nne za nomino hupangwa katika vikundi mbalimbali. Vikundi hivi vya nomino ndivyo viitwavyo ngeli za Kiswahili.

5. Nomino za makundi

mifano

Bunba la nyuki, Bunda la noti, Funda la maji, Msitu wa miti n.k.