Maneno ya kuelezea hali

Maneno ya kuelezea hali au hisia mbalimbali

  • Hisia za woga

- Kijasho chembamba kilinitoka kwapani: k.m. Nilipomwona simba kijasho...

- Nilitetemeka kama unyasi nyikani wakati wa tufani.

- Nilishika roho mkononi.

- Moyo ulinipapa kama kwamba ulitaka kufunguliwa utoroke.

- Moyo wangu ulibadilika ukawa kama wa kuku.

- Nywele zilinisimama timtim.

- Malaika yalinisimama.

- Viguu vilishindwa kunibeba.

- Macho yalinitoka pima mithili ya panya mtegoni.

- Nilitetemeka kama mbwa mbele ya chatu.

- Nilishindwa kuongea nikawa kama mja aliyeng’olewa ulimi.

- Ulimi uliniganda kinywani mwangu.

 

  • Hisia za mshangao au mshtuko

- Nilipigwa na butaa chakari.

- Nilikenua kinywa kwa mshangao.

- Nilibaki pale bila kuondoka kama kwamba nilikuwa nimepandwa ….

- Ilinibidi nijichune kuhakikisha sikuwa ndotoni. Niliduwaa na kubung’aa. Sikuyasadiki masikio yangu niliposikia….

- Niliyatumbua macho yangu kwa mshangao.

- Nilishtuka mithili ya mtu aliyepigwa ghafla kwa barafu usoni. Sikuyaamini macho yangu nilipoona ….

- Moyo uliniatuka …

 

  • Kutoroka hatari fulani

- Nilisema mguu niponye …

- Nilitundika miguu mabegani …

- Nilichana mbuga mithili ya mja aliyekimbizwa na shetani.

- Niliuponda wa fisi kuyanusuru maisha yangu.

- Nilitimua mbio mithili ya mwanambuzi amwonapo mbwa mwitu.

- Niliyazingatia ya wahenga kuwa kwa mwoga huenda kicheko ilhali kwa shujaa huenda kilio.

- Nilitoka shoti kama panya amwonapo paka.

- Niliyafuata ya wahenga kuwa, kunguru mwoga hukimbiza mbawa zake.

 

  • Hisia au hali ya simanzi

- Nilijishika tama ...

- Moyo ulinishuka ...

- Nilizama katika lindi la simanzi ...

- Nilikumbwa na ukiwa mithili ya mfiwa ...

- Niliangua kilio cha simanzi …

- Nilitumbukia kwenye bahari ya majonzi...

- Hisia za hasira Nilipandwa na mori …

- Nilipandwa na ghadhabu …

- Damu ilinichemka …

- Nilipandwa na madadi.

- Hasira zangu zilipita zile za mkizi.

- Nilikuwa na mafutu mithili ya simbabuka aliyejeruhiwa.

- Jambo hilo lilinikata ini.

 

  • Hisia za faraja

- Niliingiwa na furaha na buraha.

- Nilikuwa na furaha ghaya.

- Niliogelea kwenye bahari ya furaha.

- Nilifurahi upeo wa furaha yangu.

- Nilikuwa na faraja mithili ya kibogoyo aliyeota meno; tasa aliyepata mtoto; kiziwi aliyepata uwezo wa kusikia………

  • Hisia za kuhangaika

- Nilitapatapa mithili ya samaki atolewapo majini …

- Nilihangaika mithili ya ndege aliyetumbukia mtegoni …

- Niliriyariya kama nzi utandoni mwa buibui …

- Nilitapatapa mithili ya nondo atumbukiapo motoni …

 

  • Nguvu na umbo kubwa

- Gimba la mtu Mtu wa mataaluma manne Tambo la mtu Pandikizi la mtu Mtu wa miraba minne.

 

  • Hali ya unyonge

- Gofu la mtu Ametokwa na mabebe Fremu ya mtu Mabega yamemwanguka kama mkongwe.

- Amekonda na kukondeana Mabaki ya mtu Amebaki mifupa Mja huyo ni kifefe Ameregea parafujo za mwili. 

 

  • Hali ya umaskini

- Asiye na mbele wala nyuma.

- Umaskini wa sina sinani/hana hanani/huna hunani/hawana hawanani, nk.

- Hana/Huna/Hamna/Sina/Hatuna bee wala tee.

- Umaskini kupindukia.

- Si wa koleo si wa mani Nimetumbukia katika lindi la ufukara.

- Umaskini umemlemaza.

- Maskini hohehahe.

- Kwake hakufuki moshi.

- Hajiwezi hajimudu kutokana na uchochole.

- Si lolote si chochote.

 

 

  • Hali ya ugonjwa

- Muwele hajijui hajitambui.

- Mgonjwa si wa uji si wa dawa.

- Muwele si wa maji si wa uji Hajui aingiaye wala atokaye.

- Si hayati si mamati/si hai si mahututi.

- Mguu mmoja u kaburini, mwingine kitandani.

- Yeye yuko katika pumzi zake za mwisho.

- Anachungulia kaburini.

- Huenda akafa leo kesho kutokana na ugonjwa.

- Kifo kinamkodolea macho.

- Yuko hoi bin taabani.

- kwa maradhi.

- Siwa ulaji siwa malazi

 

  • Kitendo cha kufa kwa mtu

- Kuipa dunia mkono wa buriani.

- Kwenda jongomeo/ahera.

- Kuaga dunia

- Kuionyesha dunia kisogo

- Ni mwenda zake

- Kutangulia mbele ya hukumu/haki

- Kwenda kuzimuni

- Kufuata njia ya marahaba

- Kukata kamba

 

  • Hali ya utajiri/ukwasi wa mali

- Kuwa na mfuko mzito

- Ananuka pesa

- Ni mkwasi wa wakwasi

- Ni mtu aliye na nafasi yake katika jamii

 

  • Hali ya kupenda (kitu/mtu/jambo) sana

- Amekuwa mtumwa wa ------mf.

- Amekuwa mtumwa wa mchezo wa bao.

- Haoni hasikii Amezama katika mapenzi

- Ametekwa bakunja na -----

- Amepumbazwa na -----

- Hajijui hajielewi kutokana na mapenzi ya ----

 

  • Umuhimu wa kitu/mtu/jambo

... ni ufunguo k.m Elimu ni ufunguo wa maisha ya ufanisi. ... ni shina k.m. Kilimo ni shina la uchumi wetu.

... ni uhai k.m Maji ni uhai kwa binadamu.

... ni uti wa mgongo k.m. Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu.

... ni nguzo thabiti. k.m. Mama huyo ni nguzo thabiti ya aila hiyo

... ni mwangaza maishani. ... hewa ya kupumulia k.m. Daktari huyo amekuwa kama hewa ya kupumulia kwa wana kaya hao.

 

  • Hali ya kupigwa sana

- Nilipata pigo la kifo.

- Nilipigwa nusura nielekezwe jongomeo.

- Nilipigwa mithili ya jamvi linapokung’utwa.

- Nilipigwa kitutu/kipopo/kipapai - hali ya kupigwa na watu wengi kwa pamoja. 

 

  • Hali ya utukutu wa mtu

- Haliki hatafuniki Ametia nta maskioni mwake.

- Ametia komanga maskioni mwake.

- Haambiliki hasemezeki

- Amekuwa cha kuvunda kisicho na ubani.

- Amekuwa chombo cha kuzama.

- Yeye ni sikio la kufa lisilosikia dawa wala kafara.

- Hasikii la mwadhini wala la mteka maji mskitini.

 

  • Hali ya kuaibika au kuaibishwa

- Nilivuliwa nguo Nilipakwa jivu/matope/mavi.

- Nilikosa uso Nilitamani ardhi ipanuke inimeze niondokee aibu ile

- Nilitamani kuota mbawa nipae angani niitoroke fedheha ile

 

  • Uzuri wa maumbile ya mja

- Yeye ni malaika

- Mavazi yake yanamchukua

- Ameumbwa akaumbika

- Ni mfua uji Macho ya chawa

- Amevaa meli mpya

- Meno ya bisi

- Meno ya mchele

- Macho ya gololi

- Macho ya kikombe

- Midomo ya wekundu wa ini

- Mwanya wa kuvutia

- Shingo ya upanga

 

  • Hali mbaya ya mtu, k.m. uchafu

- Ana nywele kama dhikiri ya nzi.

- Mchafu kama kilihafu/kisafu/fugo.

- Kutoa kibeberu.

- Matongo machoni.

- Dovuo mdomoni/mashavuni.

Ngeja menoni.

Udenda midomoni