Mahitaji ya uandishi

- Katika shule ya msingi,  mwanafunzi huhitajika kuandika insha mbalimbali.

- Zipo aina kadhaa za insha ambazo mwanafunzi anatakiwa kuandika.

- Ili mwanafunzi aweze kuandika insha hizo vizuri, sharti aelewe na azifuate sheria fulani.

 

 Mahitaji ya jumla ya uandishi wa insha ni:

  •  Hati nzuri inayosomeka kwa urahisi.

  •  Urefu wa kutosha wa insha.

  •  Lugha sanifu isiyo na makosa ya kisarufi.

  •  Matumizi mazuri ya msamiati.

  •  Upambaji wa lugha kwa kutumia fani mbalimbali kama vile methali, istiara n.k.

  •  Mawazo mazito na yanayotiririka vizuri.

  •  Sentensi fupi fupi zinazoeleweka.

  •  Uzingatiaji wa mada husika.

  •   Kutumia mbinu mbalimbali kama vile taharuki ili kuvutia msomaji wa insha.