KCPE 2005 INSHA

Mtungo wa Kwanza

Mwandishi huyu amejaribu kuandika Kiswahili lakini amepotoka kwa mada, kazi yake haina uakifishaji hivyyo sentensi zimeingiliana na amefanya maosa mengi zaidi ya kisarufi na tahajia.

Alama iliyotunzwa  =  09

Mtungo wa Pili

Huyu mtahiniwa amejitahidi sana kufuata mada. Ila yake kubwa ni kutoakifisha kazi yake. Ametumia herufi ndogo  badala ya kubwa,akafuliliza badala ya kutua mwisho wa sentensi. Amefanya makosa mengi ya kisarufi, tahajia na hata msamiati. Katikati kueleza kisa chake pia amejikinza mwenyewe kwa kueleza kuwa alianguka kutoka ilhali hapo mbeleni ameeleza kuwa ni rafiki yake aliyekuwa juu yeye akiwa chini.

Alama iliyotunzwa   =  18

 Mtungo wa Tatu

Ijapokuwa mwandishi huyu amejaribu kuandika insha yake vizuri kwa kutumia lugha tamu ya tamathali na semi, hoja zake  na hasa maudhui ya insha hayaanzi kujitokeza mapema. Amefanya makosa ya sarufi, hijai na msamiati.

  • 'Nilitanabai' badala ya 'nilitanabahi'
  • 'Nilipofika karibu na maskanini mwao' badala ya 'nilipofika karibu na maskani yao'
  • 'Mwadini' badala ya Mwadhini'

 Alama iliyotunzwa   =  26

Mtungo wa Nne

Mtahiniwa amedokeza hali ya 9 (kisa) insha yake kuanzia mwanzo. Hali ya kutotulia imetanda katika insha nzima. Haya ndiyo yanayotarajiwa kulingana na kidokezo alichopewa. Makosa ya hapa na pale ya sarufi na hijai yametokeza. Hati ya mtahiniwa inasomeka bila kumtatiza msomaji.

Mfano:

'nilipouwasha' taa badala ya 'nilipoiwasha taa'

'nimimi' badala ya 'ni mimi';

'maututi' badala ya 'mahututi';

'gamani' badala ya 'ngamani';

'siku hio' badala ya 'siku hiyo';

Alama iliyotunzwa  =  32