Maswali kadirifu

Jibu maswali yafuatayo

1. Ufisadi na uhalifu katika nchi hufaa kudhibitiwa na wizara gani?

2. Haki na ajira za watoto zinafaa kusimamiwa na wizara ipi?

3. Ni wizara ipi inayowajibika kutoa miongozo na kusimamia sera za uadilifu na kuimarisha udugu, uzalendo, ujamaa na mapenzi kati ya jamii nchini?

4. Ni wizara gani inayohusika na utunzaji wa mazingira nchini?

5. Ni wazira gani inayoshughulikia maswala ya wafungwa nchini?

6. Ustawi wa lugha ya Kiswahili kama chombo cha elimu , muungano wa kitaifa na mbinu za maelewano hupaswa kuzingatiwa na wizara gani hasa?

7. Ni wizara ipi au zipi hufaa kusimamia vipindi vya redioni au runinga ili kuhakikisha kuwa havikiuki mipaka ya maadili na kupotosha au kuchafua fikra za jamii hasa kuwapotosha vijana?

8. Shughuli za mahakama zimo katika wizara gani?

9. Wageni wanaoingia nchini hupaswa kuhudumiwa na wizara gani?

10. Chuo za umma na za kibinafsi zinahudumiwa na wizara gani?