Mazoezi mseto

A. Vipange vifungu vifuatavyo kwa utaratibu ufaao

1. Kuinjika, kuepua, kukoka, kutokosa.

2. Kukaanga, kutoa matumbo, kupara, kupakua.

3. Kulima, sesa, kupalilia, kulima matuta, kuchoma.

4. Kung’oa visiki, kufyeka, kupanda, kunyunyizia.

5. Kukata rufaa, kutiwa mbaroni, kukata kesi, kusoma mashtaka.

6. Kuhojiwa, kusoma, kuajiriwa, kupasi.

7. Alasiri, macheo, machwa, adhuhuri, alfajiri.

8. “Wanafunzi wenzangu, mgeni mheshimiwa, wazazi, mwalimu mkuu na walimu, hamjambo”

9. Kukaribishwa kiti, kupokewa mzigo, kupokelewa.

10. Kuwa mvuke, kuganda, kuchemka, kuyeyuka.

11. Kuota, kunawiri, kupanda, kuchipuka.

12. Sekondari, chekechea, msingi, chuo.

13. Nahodha, kuli, baharia, serahangi.

14. Shahada, chanda, gumba, cha kati.

 

B. Teua jina baki katika kila orodha.

1. Mfarika, fahali, beberu, mvuli, mfalme.

2. Urujuani, nili, zebaki, samawati, zambarau.

3. Siki, tui, nanasi, masala, tangawizi.

4. Manukato, marashi, samli, udi.

5. Kipepesi, uyoka, barua pepe, rununu.

6. Faini, utotole, ngawira, kiingilio.

7. Kiharusi, shurua, ndigana, pepopunda.

8. Mche, hisbati, kipenyo, kiegema.

9. Mchoo, gharika, masika, kiangazi.

10. Kulungu, kasuku, kanu, chiriku.

11. Paa, dari, kiuno, ndoo.

12. Kicha, kikoa, koa, chano.

13. Bwelasuti, kanzu, kaptula, sweta.

14. Zeriba, kichuguu, kiota, kitotoa.

15. Chuma, vuna, rina, chuna.