Maswali kadirifu

A. Jibu maswali yafuatayo kwa kutumia maneno haya:

riahi, ukambi, hijabu, kipukusa, nyungunyungu, pepopunda, kifaduro, kekevu, kiwe, kiharusi, ngiri, nyongea, pumu, koyo, kichocho, kidingapopo, waba, kipwepwe, ukwasu, mjusi.

 

1. Kwikwi isababishwayo na kiungulia huitwaje?

2. Ugonjwa wa kupooza viungo vya mwili na kufa kwa hisia huitwa?

3. Homa ya kurudiarudia huitwa ________.

4. Ugonjwa wa kutoona usiku ni _____________.

5. Kuvimba miguu ya mjamzito ni ____________.

6. Ugonjwa wa kutoka damu puani ni ____________.

7. Ugonjwa wa kuambukiza wa kukohoa sana na kutoa sauti kama filimbi ni __________.

8. Ugonjwa wa ngozi uletwao na chawa ambao husababisha madoa mekundu ni ________.

9. Ugonjwa wa kukojoa damu unaoletwa na vidudu kwenye maji yaliyotuama ni

10. Maradhi ya kuvimba ufizi ni ____________.

 

B. Tumia kamusi ili utoe maelezo ya msamiati ufuatao.

 • hospitali
 • zahanati
 • wadi tembe
 • plasta
 • bendeji
 • machela
 • kipimamwili
 • kipimamajoto
 • sirinji
 • maabara
 • mualisaji
 • koleo
 • mkunga
 • muuguzi

C. Je tunatibu mgonjwa au tunatibu ugonjwa ? Jadili

 

D. Eleza maradhi yafuatayo ni yapi?

1. Kichaa cha mbwa.

2. Mbano wa akili.

3. Utandu ufunikao ubongo.

4. Kichaa cha ng’ombe.

5. Kimeta

6. Chovya

7. Choa

8. Dege

9. Homa ya ndege

10. Kikohozi

 

E. Kamilisha sentensi kwa kutaja jina la maradhi.

1. Ugonjwa wa kupooza huitwa _____.

2. Ugonjwa unaoambukizwa na viroboto wa panya huitwa _____.

3. Ugonjwa wa kualalalala unaoambukizwa na pange,chafuo au mbung'o huitwa _____.

4. _____ ni homa iletwayo na mbu.

5. _____ ni ugonjwa wa kuendesha na kutapika.

6. Upungufu wa kinga mwilini ni _____.

7. Magonjwa ya zinaa ni kama vile _____ na _____.

8. Maradhi ambayo mgonjwa hukohoa damu huitwa _____.

9. Uele uletwao na uhaba wa lishe bora hususan proteni huitwa _____.

10. Uele wa kutabawali damu ambao husababishwa na konokono huitwa _____.

 

F. Toa maelezo kuhusu maradhi haya.

 1. safura
 2. bolisukari\tetekuwanga
 3. pepopunda
 4. ndui
 5. kichomi
 6. surua
 7. mnoga
 8. ukoma
 9. kimeta