Maswali kadirifu

A. Andika majibu mwafaka kufuatana na maelezo.

 1. Kiungo kinachosafisha ngeu huitwa _____.
 2. Wingi wa ubongo ni _____.
 3. Mfupa wa mabegani huitwa _____.
 4. Mfupa unaoshikilia meno kinywani huitwa _____.
 5. Ndege hutumia makacha naye mtu hutumia _____.
 6. Kiungo kinachopiga damu ienee kote mwilini huitwa ____.
 7. Nyama laini ya mgongoni huitwa _____.
 8. Utumbo mwembamba huitwa _____.
 9. Mfuko unaohifadhi mkojo huitwa ____.
 10. Kiungo kinachogandamana na utumbo kwa upande wa kushoto huitwa ____.
 11. Sehemu ya kupitisha chakula  huitwa _____.
 12. Mfereji wa pumzi huitwa ____.
 13. Sehemu iliyoko chini ya kitovu huitwa _____.
 14. Meno huota kwenye _____.

 

B. Zikamilishe methali zifuatazo kwa kutumia majina haya ya viungomwili vya nje.

Miguu, kisogo, pua, kiganja, shingo, sikio, kinywa, mgongo, mkono, kichwa, viganja, nyonga, nywele, kidevu

 

1. ___________ ya kuitikiza sio uchungu.

2. ___________ hubeba vyombo, roho hubeba mambo.

3. ___________ kamwambia ndevu kila mtu apataye huwa mwerevu.

4. ___________ jumba la maneno.

5. Masikio hayapiti ___________

6. ___________ la kufa halisikii dawa.

7. Kofi hazilii ila kwa ___________

8. Mpa ___________ si mwenzio.

9. ___________ hayana pazia.

10. Mpiga ngumi ukuta huumiza ___________ wake.

 

11 ___________ mtupu haurambwi.

12. Vita havina ___________.

13. ___________ mmoja haubebi mwana.

14. Mwana hutazama _________ cha nina.

15. Akimbiaye huagana na ____________.

16. ________________ ni shajara.

17. Akili ni______________ kila mtu ana zake.

18. ___________ alichonyia mwana huoshwa hakitatwi.

19. Mtembezi hula ___________ yake.

20. Kata ___________ uunge wajihi.