Maswali kadirifu

Teua majibu sahihi ya maswali yafuatayo

kitara, kisiki, kushika ardhi, hori, fuko, kucheua, samadi, ulingo, kuatamia, miche, kupogoa, kuvuna, winga, kupandikiza, kitalu makoongo, kunyauka, matanda, kunyonyoa pepea.

 

1. Sehemu kuku anapotagia mayai.

2. Chombo cha kulishia wanyama.

3. Mbolea itokanayo na kinyesi cha wanyama hususan wacheuao huitwa ________.

4. Ile hali ya kutafunatafuna chakula kitokacho tumboni kamavile wafanyavyo mbuzi huitwa ________.

5. Kitendo cha kuwafukuza ndege na wanyama wengine ili wasiharibu mazao shambani ni ________.

6. Jukwaa la kulindia shamba ili mazao yasiharibiwe na wanyama huitwa _____.

7. Mashimo ya kupanda mbegu.

8. Kile kitendo cha kuku “kuyalalia” mayai ili yaanguliwe huitwa _____.

9. Kupunguza matawi mtini ni _____.

10. Mimea michanga huitwa _____.

 

11. Kung’oa mimea michanga na kupanda sehemu nyingine ni _____.

12. Sehemu ya kukaushia mbegu.

13. Kishamba cha kukuzia miche kabla haijapandwa huitwa _____.

14. Hali ya mmea kufifia kutokana na joto au ukame ni ____.

15. Kipande cha mti kinachobaki chini ya ardhi baada ya mti kukatwa ni _____.

16. Hali ya mmea kuendelea kukua baada ya kupandwa ni _____.

17. Kitendo cha kutoa mazao/mavuno shambani ni _____.

18. Mbolea itokanayo na mlundikano wa majani makavu kwenye shina la mmea huitwaje?

19. Hali ya kuyaweka matunda palipo na joto ili yawe mabivu ni ____.

20. Kitendo cha kuondoa nyoya za kuku ni _____.

Taja kazi ya vyombo vifuatavyo. 

1. Sepetu                   7. Reki

2. Jembe                    8. Panga

3. Muundu                 9. Tingatinga

4. Haro                      10. Fyekeo

5. Shoka                    11. Plau

6. Glovu                     12. Dodoki