Maswali kadirifu

Toa majibu sahihi.

mtetezi, mhajiri, mhaini, mgombezi, mgunduzi, wakimbizi, mhafidhina, jasusi, mwanamgambo, karagosi.

 

1. Mtu ambaye amehamia mahali kutoka sehemu nyingine ni ________.

2. Mtu ambaye amedhihirisha jambo ambalo halikuwa likijulikana ni ________.

3. Mtu anayefanya njama za kupindua serikali yake ni ________.

4. Mtu anayemtetea mwengine ili apate haki yake na asionewe ni ________.

5. Mtu anayewania nafasi ya uongozi kwa kushindana na wengine ________.

6. Mtu ayapingaye mabadiliko huitwa ________.

7. Watu waliotumiwa na wakoloni kuwagandamiza Waafrika wenzao enzi za ukoloni wanaweza kuitwa ________.

8. Kutokana na kudidimia kwa usalama, Juma na wenzake wamejitolea kulinda kijiji chao. Tunaweza kuwaita ________.

9. Mzee huyo alitiwa mbaroni akipeleleza kambi za wanajeshi wetu. Yeye ni ________.

10. Kutokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, nchi yetu ilipokea ________ wengi kutoka nchi jirani.