Maswali kadirifu

 

A. Taja rangi ya vitu vifuatavyo.

 • chai ya mkandaa
 • ini
 • limau bivu
 • mawingu
 • mbingu bila mawingu
 • mvi
 • ngeu
 • umbijani
 • dhahabu
 • masizi

 

BSehemu (i)

Hizi ni rangi gani?

 1. madharani
 2. samawati
 3. feruzi
 4. samli au siagi
 5. zambarau nyeupe
 6. damu ya mzee
 7. chanikiwiti
 8. bitimarembo
 9. buluu kolevu
 10. sorangi

Sehemu (ii) 

Chora upinde wa mvua na utaje rangi zote.