Maswali kadirifu

Zoezi katika tarakimu

A. Andika tarakimu zifuatazo.

 

1. Robo milioni.

2. Laki moja unusu.

3. Elfu tano, mia sita na sita.

4. Mia tano na tano elfu, mia nane themanini na nane.

5. Tisini na nane elfu, mia saba.

6. Elfu sitini, mia sita na sita.

7. Kumi na nane

8. Laki mbili na robo.

9. Milioni mbili unusu.

10. Robo milioni.

 

11. Robo ya laki.

12. Elfu sita na sita.

13. Milioni kumi laki saba unusu.

14. Milioni sita, mia nane na nne elfu.

15. Kumi na nane elfu.

16. Laki moja, sabini na nane elfu na kumi.

17. Kumi na saba milioni, laki nne unusu.

18. Hamsini na nne milioni.

19. Kumi na nne na nusu.

20. Themanini na nane elfu, mia moja kumi na mbili na nusu.

 

B. Andika katika nambari.

 1. Milioni kumi na moja
 2. Milioni nne, laki nne na mia nne
 3. Milioni sabini na tano,elfu kumi na tano
 4. Milioni tano,laki nne na themanini na kenda
 5. milioni ishirini na moja,laki saba na robo

 

C. Andika tarakimu hizi katika maneno.

1. 9,999

2. 999

3. 6,000,666

4. 7,703,332

5. 10,000,002

6. 5,555,555

7. 111,199,007

8. 1,111,111

10. 3,300,003

 

D. Andika katika lugha ya kawaida  tarakimu zifuatazo.

 • miteni
 • laki
 • gana
 • alfu lela ulela
 • alfeni
 • mwakani
 • korija
 • darzeni
 • lakieni
 • jozi

E. Andika kwa maneno.

1. 7.02%
2. 61.01%
3. 0.5%
4. 20 %
5. 500,000
6. 250,000
7. 50,000
8. 601,000
9. 600,001
10. 600,101
11. 21.007%
12. 36,000
13. 21,002
14. 41,414
15. 717,717,717