Maswali kadirifu

Zoezi A

Jibu maswali yafuatayo kwa kutumia maneno uliyopewa. masizi, jokofu au jirafu, mafiga au mafya, kilalio au chajio, staftahi au kisabeho, ukoko, kuteleka au kuinjika, kiporo, kepua au kudeua, masizi, mlale

1. Yale mawe matatu ya jikoni huitwa ____

2. Kitendo cha kuweka chombo kama vile sufuria juu ya moto tayari kupikia huitwa __________.

3. Ule uzi unaotokana na moshi jikoni huitwa ___________.

4. Kitendo cha kuondoa chungu jikoni ni __________.

5. Mashine ya barafu inayotumika kuhifadhia chakula au kufanya vinywaji viwe baridi huitwa __________.

6. Mabaki ya chakula kwenye chungu ni ______.

7. Chakula cha asubuhi huitwa _________.

8. Chakula kilicholala huitwa __________

9. Ungaunga mweusi unaopatikana nje ya chungu cha kupikia ni __________.

10. Chakula cha jioni huitwa __________.

Zoezi B

Jaza pengo kwa kutumia jawabu mwafaka. kudondoa, kiliungua, huandaa, kupekecha, kupasha moto, kutokota, kukoka, kumenya, mwale, kupuliza moto

1. Mama ____ chakula mezani baada ya kukipika.

2. Ilinibidi ____ maji hayo ili niyaogee kwani yalikuwa baridi kama barafu.

3. Dadangu alipomaliza ____ alipika uji wa kitinda mimba wetu.

4. Mama aliniagiza nizidi ____ ili chakula kiive haraka.

5. Baada ya chakula ____ niliuzima moto na kukiepua.

6. Baada ya ____ viazi hivyo, tuliviosha na kuvikaanga.

7. Nilipotoka shuleni, nilianza ____ mchele kisha nikauweka chunguni.

8. Baba aliamua ____ maziwa ili kutoa mtindi

9. Tulitumia alasiri yote jikoni tukipanguza ____ ulioshikilia kutani.

10. Chakula hicho ____ mpishi alipokawia kurudi jikoni kuuzima moto.

Zoezi C

Toa jibu mwafaka ili kukamilisha sentensi zifuatazo.

1. Jiko la makaa huitwa _____.

2. Chombo cha kuokea mikate ya kumimina huitwa _____.

3. Kupasha chakula moto ni _____.

4. Kifaa chaa kukunia nazi huitwa _____.

5. Chombo cha kuchujia tui la nazi huitwa kumto,kung'uto au _____.

6. Chakula kinachoganda katika kifaa kilichopikiwa huitwa _____.

7. Chakula kilicholala mpaka asubuhi huitwa _____, _____, au _____.

8. Kifaa cha kupepetea nafaka  huitwa _____.

9.Nazi iliyokunwa huitwa _____.

10.Maji meupe ya nazi huitwa _____.

 

Zoezi D

Tumia kamusi kueleza maana ya maneno haya.

1. susu

2. mchi

3. sinia

4. jirafu

5. kikaango

6. karo

7. dohani

8. birika

9. buli

10. chano

 

Zoezi E

Eleza vitendo vifuatavyo vya jikoni.

1. umuka

2. tokosa

3. chemsha

4. banika

5. koka

6. oka

7. kaanga

8. pika

9. songa

10. injika

 

Zoezi F

Ni vitu vipi hufanyiwa vitendo vifuatavyo?

Mfano: menya - viazi

  • umua
  • ambua
  • angua
  • chuna
  • para
  • pogoa
  • kokoa
  • dondoa
  • nyonyoa
  • kama