Makao

Makao ni mahali kiumbe huishi.

 

 Makao ya watu/wanadamu

- Makao ya wavulana waliotiwa jando ni kumbi.

- Rais huishi kwenye ikulu.

- Mfalme huishi kwenye kasri.

- Mtawala huishi kwenye kitala.

- Mfungwa hukaa gerezani/husuni.

- Makao ya mtu angojeaye kesi ikatwe ni mahabusi/mahabusu/rumande.

Makao ya wanyama

- Ng’ombe huishi kwenye zizi/chaa/zeriba/ buruji.

- Samaki huishi majini.

- Kasuku huishi kwenye tundu.

- Kuku huishi kwenye kizimba.

 

- Fuko huishi shimoni.

- Nyuni huishi kiotani.

- Makao ya kiwavi ni kifukofuko.

- Makao ya panzi ni nyasini.

- Konokono huishi kwenye koa/kombe.

 

- Funza huishi vidoleni.

- Mchwa huishi katika kichuguu/kidurusi/ kingulima/kishirazi.

- Jana huishi katika masegasega.

- Nyuki huishi katika mzinga.

- Buibui huishi kwenye utando/utandabui.

- Makao ya uchango ni utumbo.

Miti

- Mti ni mmea wenye shina gumu.

- Neno mti unapatikana katika ngeli ya - U - I. Mti - Miti.

 

Ndege wa mtini

- Kunao baadhi ya ndege wanaochimba mashimo mitini na kuyatumia kama makao yao. Kwa kiingereza wanarejelewa kama 'Cavity nesters'.

Mifano:-

Bundi - owl, kasuku - parrots, n.k.

 

Umuhimu wa miti

a) Makao ya viumbe kama vile wanyama na ndege.

b) Hutupa kivuli, pa kupumzika wakati wa jua kali.

c) Miti mingine hutumika kama dawa, yaani madawa ya kienyeji ambayo huyatibu baadhi ya magonjwa.

d) Huvuta mvua.

e) Hutupa mbao zinazotumika kwa njia nyingi. Kama vile kutengeneza viti, vitanda na meza.

f) Husafisha hewa.

g) Miti pia hutumika kama kuni. 

h) Wanasayansi hutumia miti au mahali pa miti mingi kama vile misitu kufanyia utafiti. Kwa mfano, aina za miti katika misitu mbali mbali duniani.

i) Miti huboresha mandhari ya nchi. 

j) Miti hutupa karatasi kutota kwa karakana.

k) Dandalo za umeme hutoka kwa miti.

l) Baadhi ya miti pia hutuzalia vyakula kama vile maembe, mapera, parachichi, paipai, machungwa, karakara n.k.