Mahali mbalimbali

 

- Kuna mahali au sehemu mbalimbali za kufanyia shughuli mbali mbali.

- Yatazame maelezo ya mahali yafuatayo.

 

1. Maktaba: sehemu ya kuwekea vitabu kwa ajili ya kusoma na kuazima.

2. Makavazi: mahali ambapo vitu vya kale huwekwa kuchunguzwa na kuonyeshwa.

3. Maabara: sehemu ya kufanyia utafiti wa kisayansi.

4. Bohari: sehemu ya kuhifadhia silaha.

5. Karakana: mahali pa kutengenezea vitu kwa mitambo.

6. Hospitalini: sehemu ya kutolea matibabu kwa wagonjwa.

7. Ufuoni/makafani: Sehemu ya kuhifadhia maiti.

8. Pambajio: sehemu katika nyumba ambapo watu hukaa kungojea zamu zao.

9. Sebule: chumba cha kupokelea wageni na cha mazungumzo

10. Hamamuni: chumba cha kuogea.

 

11. Mahakamani: Mahali ambapo kesi husikilizwa na kuamuliwa.

12. Stanini: Mahali pa kuabiria na kushikia magari ya usafiri ya umma.

13. Kivukomilia: Mahali rasmi pa kuvukia barabarani palipochorwa mistari mieupe.

14. Maegesho: Mahali speshieli pa kuwekea/kuegesha magari.

15. Korokoroni: Chumba katika kituo cha polisi cha kuwafungia washukiwa.

16. Gerezani/Husuni: Sehemu ya kufungiwa wahalifu ili kuadhibiwa warekebishe mienendo yao.

17. Rumande: Chumba katika gereaza wanapofungiwa mahabusu wanaosubiri kumalizika kwa kesi zao.

18. Maabadini: Mahali a kuabudia. 

19. Mskitini: maabadi ya waislamu.

20. Hekaluni: Maabadi ya wayahudi.

 

21. Sinagogi: maabadi ya Wayahudi.

22. Kanisa: maabadi ya Wakristo

23. Mahame: mahali palipohamwa (ganjo/tongo)

24. Kizimbani: sehemu ya mahakamani asimamapo mshtaki, mshtakiwa au shahidi wakati wa kesi.

25. Fuko: mahali kuku hutagia

26. Ghala/stoo: jengo la kuhifadhia bidhaa

27. Madobini fuo: mahali maalum ambapo madobi hufulia nguo

28. Chimbo: shimo kubwa ambapo huchimbuliwa udongo, mchanga au madini.

29. Mapokezi: ofisi ya kupokelea wageni

30. Kilinge: mahali pa uganga

  • Bohari by jicslogistic.com/warehousing/ & eLimu used under CC_BY-SA
 • Hamamuni by https://www.pinterest.com/pin/458100593327458054/ & eLimu used under CC_BY-SA
 • Image-6-Hospitali by https://www.newsecuritybeat.org/.../woman-centered-maternity-care-famil... & eLimu used under CC_BY-SA
 • image-7-Makafani by gromanmortuaries.com/ & eLimu used under CC_BY-SA
 • Karakana by www.horizontalheavens.com/WorkShop.htm & eLimu used under CC_BY-SA
 • Maabara by www.bls.gov › ... › Life, Physical, and Social Science & eLimu used under CC_BY-SA
 • Makavazi by www.kenyatoursandsafaris.com/.../113-national-museum-snake-park & eLimu used under CC_BY-SA
 • Maktaba by topics.hivisasa.com/kiambu/education/79443 & eLimu used under CC_BY-SA
 • Pambajio by https://www.pinterest.com/pin/485051822340239221/ & eLimu used under CC_BY-SA
 • Sebule by https://www.totalmortgage.com/blog/general/5-rules-for-arranging-your-living-room/27230 & eLimu used under CC_BY-SA
 • Gerezani by tuko.co.ke › Crime & eLimu used under CC_BY-SA
 • Hekaluni by https://oaklandsinai.org/History & eLimu used under CC_BY-SA
 • Image-15_Parking by https://www.flickr.com/photos/thienzieyung/6725294627 & eLimu used under CC_BY-SA
 • Kivukomilia by weburbanist.com/2012/.../10-more-creative-crosswalks-zany-zebra-crossin... & eLimu used under CC_BY-SA
 • Korokoroni by www.thejha.org/facilities & eLimu used under CC_BY-SA
 • Machakos_country_bus by ke.worldmapz.com/photo/1912_fr.htm & eLimu used under CC_BY-SA
 • Mahakamani by www.jambonewspot.com/iebc-cites-bush-vs-gore-in-defense-against-poll-... & eLimu used under CC_BY-SA
 • Mskitini by https://www.pinterest.com/inayani/beautiful-mosques-islamic-architecture/ & eLimu used under CC_BY-SA
 • Rumande by nairobiwire.com/2014/02/murder-suspects-forced-cut-remand.html & eLimu used under CC_BY-SA
 • Chimbo by knowyourmeme.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • Fuko by rationalfaith.com/2015/06/evolutions-evil-eggs/ & eLimu used under CC_BY-SA
 • kanisa by softkenya.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • madobini_fuo by en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • Mahame by www.panoramio.com/photo/87741437 & eLimu used under CC_BY-SA
 • Sinagogi by schoolwires.henry.k12.ga.us/.../Monotheistic%20Religions%20KW.pdf & eLimu used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.