Maswali kadirifu

A. Kamilisha majina ya wafanyakazi wanaoelewa.

 

1. Mtu anayefua visu huitwa _____.

2. Mtu aliye na elimu ya nyota huitwa _____.

3. Mtu anayefua mabati na vyuma huitwa _____

4. Daktari wa kuunganisha viungo vya mwili huitwa _____.

5. Anayepakia na kupakua shehena bandarini huitwa _____.

6. Mtu anayerusha ndege huitwa ____.

7. Anayejenga nyumba kwa mawe, matofali au saruji huitwa _____.

8. Msimamizi wa mabaharia huitwa _____.

9. Fundi wa mitambo huitwa _____.

10. Msimazi mkuu wa shamba huitwa _____.

11. Mwizi wa baharani huitwa _____.

12. Anayetengeneza pombe ya mnazi huitwa _____.

13. _____ ni anayepeleka barua kwa posta.

14. Mnunuzi katika mnada huitwa _____.

15. Mtu anayewafunza vijana kunga za nyumbani huitwa _____.

16. Anayehariri miswada huitwa _____.

17. Mnunuzi katika mnada huitwa ____.

18. Fundi stado wa kupiga ngoma huitwa _____.

 

B. Watu hawa hufanya kazi gani?

1. mrina
2. mkimbizi
3. katikiro
4. manamba
5. mwanazaraa
6. mpagazi
7. diwani
8. meya
9. mhazigi
10. shaha
11. msusi au msonzi
12. msukaji
13. seremala
14. mdau au mshikadau
15. saisi
16. mswawidi
17. mamantilie
18. chokorido
19. mhazili

C. Zitaje kazi za wafuatao.

 

 •  Mwalishi
 •  Sarahangi
 •  Mchuuzi
 •  Mwamizi
 •  Mfugaji
 •  Mamantilie
 •  Mlumbaji
 •  Mgema
 •  Mbunge
 •  Baharia
 •  Wakili
 •  Mjumu
 •  Diwani
 •  Mrumba
 •  Kandawala
 • Gambera

 

D. Taja watu wazifanyazo kazi hizi.

1. Aliyesomea diplomasia ni_________.
2. Mtu afanyaye utafiti wa mambo ya sayari za juu __________. 
3. Mchezaji wa mpira wa miguu ni __________. 
4. Afanyaye kazi katika meli ni __________ .
5. Achezaye michezo ya riadha ni __________.
6. Raia anayejitolea kufanya kazi ya ulinzi ni __________.
7. Askari katika jeshi la ulinzi __________.
8. Anayeshughulika na sheria ni __________.