Nomino za makundi

- Nomino za makundi hutumika kuonyeshea mkusanyiko wa nomino au nauni nyingi. 

- Nomino za makundi zinaweza kuwa za viumbe k.v. watu au vitu k.v. magari. 

 

Mifano:

 • a) Kaumu ya watu

Kaumu (i-zi): Umati wa watu fulani. 

Mfano katika sentensi: Niliona kaumu ya wafuasi katika mji.

b) Halaiki ya watu
c) Umati wa watu
d) Hadhara ya watu
e) Sisisi ya watu
f) Sufufu ya watu
g) Msafara wa watu

 

 • Mkururo wa watoto

Mkururo (u-i: mfuatano wa vitu au watu mmoja baada ya mwingine.

 

 • Mzengwe wa wagomaji

 

 • Jamii ya watu/miti/vifaranga
 • Msitu wa miti

 

 • Mlolongo wa magari, watu 

Mlolongo (u-i): mfuatano wa vitu au watu mmoja baada ya mwingine.

 

 • Thurea ya nyota

 

 • Biwi la takataka, kwekwe, magugu, simanzi.
 • Jaa la takataka, magugu, kwekwe.

 

 • Funda la maji

Funda; Ujazo wa chakula au kinywaji kwenye kinywa na kuvimbisha mashavu. Katika sentensi; Piga funda la maji.

 

 • Chemchemi ya maji. 

Chemchemi

- Chemchemi pia inaitwa bubujiko. 

- Chemchemi ni mahali maji yanapopenyea kutoka arthini. 

 

 • Jozi ya viatu, 
 • Jozi ya soksi, karata, vipuli, 

Jozi (i-zi); vitu viwili vilivyo pamoja na vinavyofanana.

 

 • Shada la maua
 • Mtungo wa maua
 • Koja la maua, mawaridi

 

 • Chane la ndizi, nafaka

 

 • Hombo la samaki.
 • Mtungo wa samaki.
 • Tumbi la samaki.

 

 

 • Doti la leso, kanga. 

- Pia gora(i-zi), kwa mfano gora ya leso. 

- Vipande viwili vya kitambaa kama vile kanga, kitenge vinavyofanana au aina moja. 

 

 • Bunda la noti, karatasi. 

 

Bunda; Fungu la vitu kama karatasi au nguo vilivyofungwa pamoja. 

 

 • Shungi/tuta la nywele. 

Shungi; nywele ndefu au manyoya yaliyotokeza mbele ya kichwa cha mtu au ndege.

 

 • Sharafa la ndevu.

 

 • Seti ya sahani, vikombe, fanicha. 

Seti; Fungu la vifaa au vitu vya aina moja vinavyohusiana katika kukamilisha shughuli fulani.

 

 • Shuke la nafaka | Shazi la nafaka.

 

 • Halmashauri ya shule.

Halmashauri ni kikundi cha watu maalumu walioteuliwa au kuchaguliwa kuelekeza jambo. Pia kikundi hiki kinaweza kurejelewa kama, bodi.

 

 • Baraza la mawaziri.

Baraza (i-zi); kikundi cha watu walioteuliwa au kuchaguliwa na kupewa madaraka maalum.

 • Topa la vitabu

 

 • Mnofu wa nyama

Mnofu (u-i); nyama isiyo na mifupa au mwiba.

 

 • Tanuri la chokaa

Tanuri (li-ya); jiko lililojengwa ambalo linatumika kuchomea vitu k.v. chokaa, vyombo vya udongo au mikate.

 

 • Tonge/donge la ugali.

Donge (li-ya); Kitu cha mviringo kilichoshikamana. Tazama pia neno bonge, tufe.

 

 • Tone la damu

Tone (li-ya); sehemu ndogo ya kitu kiowevu kinachondondoka. Matone ya mvua, maji, dawa, kemikali, na kadhalika.

 

 • Kifurushi cha nguo

Kifurushi (ki-vi); vitu vilivyofungwa pamoja kwa karatasi na gundi, nguo au kamba.

 

 • Karne ya miaka

 Karne (i-zi); Muda wa miaka mia moja. 

 

 • Korija ya shanga, blanketi

Korija (i-zi); vitu vya aina moja, kama vile miti, shanga, au nguo vikiwa ishirini ishirini pamoja.

 

 • Kundi la fisi, ndege n.k.

Kundi (li-ya); mkusanyiko wa vitu, watu au wanyama.

 

 • Misitu ya miti

Misitu (u-i); Mahali penye miti mingi, mikubwa na midogo, vichaka na hata nyasi.

 

 • Kanzi la maharagwe, mahindi, ngano, mpunga.

Kanzi; chakula kilichpikwa pamoja kwa kuchanganywa mchele, pojo, bizari, nyama, pilipili, na samli.

 

 • Kichaka cha miti

Kichaka (ki-vi); mahali penye miti mifupimifupi iliyoshonana na nyasi, miiba na kadhalika. Pia huitwa kituka

 

 • Robota la pamba | Robota la mitumba.

Robota (li-ya); mtumba mkubwa wa bidhaa uliofungwa pamoja kama vile nguo, pamba ili kusafirishwa.

 

 • Korija la magunia/mablanketi/vitambaa

Korija (i-zi); vitu vya aina moja, vikiwa kwa idadi ya ishirini.

 

 • Jora la bafta/vitambaa/vitenge

Jora (li-ya); bunda la kitambaa lenye urefu wa mita 27. 

Mfano, mtumba wa majora.

 

 • Kopo la uji/chai/kahawa

Kopo (li-ya);

1. Chombo cha chuma au bati, kinachotumiwa kuchotea kitu au kutilia kitu. 

2. Bomba la kuteremshia maji kutoka kwenye dari la nyumba. 

3. Hutiwa pembeni mwa bati ili kukingia maji ya mvua. 

 

 • Darzeni ya mayai/matunda/vikombe na kadhalika. 

Darzeni/dazeni (i-zi); Jumla ya vitu kumi na viwili.

 

 • Kigaro cha wasingiziaji/wasengenyaji/wazushi n.k.

Kigaro (ki-vi); mkusanyiko wa watu wenye nia ya kumsema mtu vibaya au kumpangia jambo la kumdhuru, au kumdharau na kumfedhehi.

 

 • Jopo la waandishi | Paneli ya majaji

Jopo (li-ya); Kikundi cha watu waliokusanyika pamoja ili kufanya kazi maalum. Pia paneli

 

 • Baraza la wazee

Baraza (i-zi); kikundi ya watu waliochaguliwa na kupewa madaraka maalum ili kutekeleza majukumu fulani.

 

 • Genge la vibarua/wezi. 

Genge (li-ya); kundi la watu wanaofanya kazi pamoja. 

 

 • Pakacha la matunda (kikapuni)

Pakacha (li-ya) - kikapu kilichosukwa kwa makuti ya mnazi.

 

 • Kichala cha matunda (mtini) | Kichaa cha matunda, mboga, funguo n.k.

Kichala (ki-vi); Kitawi cha matunda yaliyo mengi pamoja. Kichala pia huitwa kichaa.

 

 • Kifungu cha matunda (sokoni), viazi, ndizi, sukumawiki

Kifungu (ki-vi); kipimo cha vitu vilivyotengwa pamoja. Kama vile matunda na viazi.

 

 • Kikonyo cha zabibu

Kikonyo (ki-vi); - kishina cha tunda au ua ambacho hujishikilia kwenye tawi la mti.

 

 • Tita la nguo, kuni.

 

 • Mzinga wa nyuki

 

 • Bumba la nyuki.

Maana ya bumba

1. Mfuko mdogo, wa majani ya chai, wa tumbako.

2. Fungu la vitu au wadudu kama vile kikundi cha nyuki waliosongamana na kushikana sana. 

 • Bumba la majani
 • Bumba la tumbaku, bumba la nyuki

 

 • Mkungu wa ndizi.

Mkungu (i-zi); sehemu ya mgomba yenye ndizi.

 

 • Chano la chakula.

Chano (ki-vi); sinia kubwa la ubao la kupakulia chakula.

 

 • Wingu la moshi, vumbi, nzige. 

 

 • Kikoa cha waimbaji/wachezaji.

Kikoa (ki-vi); umoja au ushirika wa watu wanaofanya mambo yao au kazi zao kwa zamu.

 

 • Kipeto cha barua

Kipeto

1. Kifurushi kilichfungwa vizuri ili vitu vilivyo ndani yake visisambaratike.

2. Gunia la vitu.

 

 • Safu ya watu/milima/nyumba.

Safu (i-zi); mstari aghalau wa watu waliojipanga mmoja nyuma ya mwingine.

 

 • Kilinge cha wachawi.

Kilenge (ki-vi); mahali pa uganga.

 

 • Kikosi cha askari, jeshi la askari.

Kikosi (ki-vi); mkusanyiko wa askari zaidi ya elfu moja, huwa chini ya meja. • umati by https://www.crowdrise.com/rebuildingthevillage & eLimu used under CC_BY-SA
 • misitu-ya-miti by www.geograph.ie/photo & eLimu used under CC_BY-SA
 • mkururo-wa-watoto by allafrica.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • mlolongo-wa-magari by www.geograph.ie/photo & eLimu used under CC_BY-SA
 • mzengwe-wa-wagomaji by tuko.co.ke & eLimu used under CC_BY-SA
 • 5cfc469d-9b58-4d29-9eb4-64b1d5318a5d by https://www.pinterest.com/pin/481955597595521659/?lp=true used under CC_BY-SA
 • bfa46ef6-dd94-4c8f-8c22-f3ec2c00a468 by https://www.flickr.com/photos/pokoroto/2481662783/ used under CC_BY-SA
 • d4ed82a9-f464-4e68-ac4c-3d09d80a2d63 by https://www.shutterstock.com/search/pile+of+rubbish used under CC_BY-SA
 • thurea-ya-nyota by phys.org › Astronomy & Space › Astronomy & eLimu used under CC_BY-SA
 • chane-la-ndizi by https://wall.alphacoders.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • jozi-ya-viatu by en.wikipedia.org & eLimu used under CC_BY-SA
 • shada-la-maua by www.pinterest.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • 2cb0efda-7eb9-4647-a46d-aabaf560f707 by https://picclick.com/Kenya-5-Note-Set-50-to-1000-Shillings-233273316277.html used under CC_BY-SA
 • 480b37c5-33e9-4816-a46e-374a13f0809c by http://pascapanen.litbang.pertanian.go.id/actual.html?type=news&id=117 used under CC_BY-SA
 • 72a0cd15-aad8-41b6-80dd-82ccbd4692e0 by e-Limu used under CC_BY-SA
 • 7cb3d928-2029-44bb-869f-8cdaaf9a6163 by http://metawatch.info/design/ used under CC_BY-SA
 • hombo-la-samaki by nourishtheplanet.com & eLimu used under CC_BY-SA
 • 2e9aa327-b6a8-4012-ad34-2c8f98c020fd by http://www.thecrownmarket.com/?attachment_id=2924 used under CC_BY-SA
 • topa-la-vitabu by www.thinkinclusive.us & eLimu used under CC_BY-SA
 • 67581b4b-e7e6-4999-9afb-9320d8fb1cf6 by https://www.countryliving.com/gardening/garden-ideas/g27104528/low-maintenance-bushes-shrubs/ used under CC_BY-SA
 • c1c17eeb-36be-4326-a3bd-00204ea5c1db by https://www.displayfakefoods.com/store/pc/Egg-Dozen-Brown-In-Carton-p214.htm used under CC_BY-SA
 • dc7c786b-044b-4e65-b8ea-10c0b65a0eb5 by https://www.nation.co.ke/news/Interviews-for-judges-enter-second-week/1056-5169236-mpyt0xz/index.html used under CC_BY-SA
 • ed933683-c60f-4784-ba22-1deb8e0a2a6b by elimu used under CC_BY-SA
 • 382f8370-892f-48e6-b90b-48932f8b04f6 by elimu used under CC_BY-SA
 • 585aa72b-5bdb-4301-8055-b9e1ae7ca6b1 by https://www.turbosquid.com/3d-models/3d-model-kindling-wood/1046984 used under CC_BY-SA
 • 7188b2f5-73e6-4b87-9f8e-fb5cac2d1396 by https://www.freepik.com/free-photos-vectors/grape-branch used under CC_BY-SA
 • 9cebd31c-a5bd-4c3e-a3eb-4f0ee43edf29 by e-Limu used under CC_BY-SA
 • 7ed20461-925d-4edf-b70b-ba4fa071b795 by https://www.shutterstock.com/video/search/smoke-coming-out-of-exhaust?page=2 used under CC_BY-SA

 • Creative Commons License
  All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.