Maswali kadirifu

A. Jibu maswali haya ya misimu kwa usahihi.

 

1. Msimu wa jua kali huitwa ____.

2. Msimu wa mvua nyingi huitwa _____.

3. Msimu wa mvua ndogo ndogo huitwa _____ au _____.

4. Msimu wa baridi shadidi huitwa ______ .

5. Hali ya nchi kukauka kwa kukosa maji,malisho na mavuno huitwa _____.

6. Kishuka huliwa wakati wa?____________

7. Kiporo huliwa lini? _______________

8. Jua huchwa lini? _________________

 

B. Toa maelezo mafupi kuhusu:

  1. machipuko
  2. mapukutiko
  3. yahom
  4. bamvua
  5. rasharasha
  6. manyunyu
  7. kusi
  8. kaskazi

 

C. Zipange nyakati hizi ipasavyo kwa mfululizo bora

1. adhuhuri                      2. jioni

3. alasiri                          4. mawio

5. magungulianyama      6. mafungianyama

7. usiku mchanga            8. usiku mkuu

9. machweo                   10. asubuhi