Saa

- Saa ni chombo ambacho hutuonyesha wakati.

- Chombo hiki kwa kawaida huwa na akrabu.

- Akrabu ni sawa na vijiti. Kuna akrabu fupi ionyeshayo saa (dakika sitini) na ile ndefu ionyeshayo dakika. Ya tatu ambayo pia ni ndefu, huonyesha sekunde.

- Akrabu fupi ikamilishapo mzunguko mmoja huwa imechukua muda wa saa kumi na mbili.

- Kwa hivyo basi, akrabu hii fupi huchukua muda wa saa moja “kwenda” kutoka nambari moja hadi ile nyingine. k.m. kutoka moja hadi mbili.

- Nayo akrabu ndefu ya dakika, huchukua dakika sitini au saa moja kufanya mzunguko mmoja.

- Ile ndefu ya sekunde (nukta) hutumia dakika moja (sekunde sitini) kuzunguka mduara mmoja.

 

Mchoro wa saa.

 

- Siku nzima huwa na masaa ishirini na nne.

- Yaani saa kumi na mbili usiku kucha na saa kumi na mbili mchana kutwa.

- Kipindi cha saa moja huwa na dakika sitini.

- Nusu saa ni sawa na dakika thelathini.

- Robo saa ni sawa na dakika kumi na tano.

- Dakika moja nayo huwa na sekunde sitini.

- Sekunde pia huitwa nukta.

 

Usomaji wa saa kimataifa

Tuangaliapo saa, hatuna budi kufuata mtindo wa Kizungu ambapo akrabu ile fupi ielekeapo kwenye nambari moja humaanisha ni saa saba.

Ielekeapo kwa nambari mbili huwa ni saa nane n.k.

 

 Usomaji wa saa kwa Kiswahili

Iangalie michoro hii ya saa inayosomwa kwa Kiswahili:

 

- Iwapo saa imeandikwa kwa tarakimu, tutaisoma tarakimu ile vile tunavyosoma uso wa saa.

- Iangalie mifano ifuatayo kwa makini.

- Saa 7.15 -Saa saba na dakika kumi na tano au saa saba na robo wala si saa moja na robo.

- Saa 10.30 -Saa kumi na nusu, au saa kumi unusu au saa kumi na dakika thelathini.

- Saa 4.30 - Saa nne unusu.

- Saa 1.15 - Saa moja na dakika kumi na tano au saa moja na robo.

- Saa 9.45 - Saa tisa na dakika arobaini na tano au saa kumi kasorobo.

 

- Iwapo zimepita dakika thelathini, badala ya kusema dakika thelathini, unaweza kusema nusu. k.m. Saa 12.30 – unaweza kusema saa kumi na mbili unusu au saa kumi na mbili na nusu.

- Iwapo zimepita dakika kumi na tano, unaweza tumia robo badala ya dakika kumi na tano. k.m.

- Saa 2.15 – saa mbili na dakika kumi na tano au saa mbili na robo.

- Iwapo zimepita dakika arobaini na tano, unastahili kutumia kasoro robo au kasorobo. k.m. Saa 6.45 – saa saba kasorobo. Maana yake ni kuwa, bado dakika kumi na tano (robo saa) itimie saa saba.

 

Kujumlisha na kutoa wakati/saa

Unapojumlisha saa, sharti ukumbuke kuwa, saa moja ina idadi ya dakika sitini.

Kwa hivyo basi, ukijumlisha dakika na zitimie sitini unastahili kuzigeuza dakika hizo sitini kuwa saa moja. Idadi hiyo ya saa moja hivyo basi uihamishe upande wa tarakimu za saa.

 

Uangalie mfano ufuatao:

Hamisi alianza safari yake saa tano na robo asubuhi. Ilimchukua dakika hamsini kufika sokoni.

Je, alifika sokoni saa ngapi? Kuanza safari 5.15 5.15 Muda safarini + 50 0.50 Wakati wa kufika 5. (6)5 5 +(6)5 6.05 Saa 5 + 65 = 5.00 + 65 = 5.00 + 1.00 + 0.05 = 6.05

Unapotoa saa, mbinu ni yiyo hiyo. k.m.

Fatuma alifika harusini saa nne na dakika kumi. Iwapo ilimchukua dakika arobaini kutembea kutoka kiamboni hadi harusini, je, alitoka kiamboni saa ngapi?

Kufika arusini 4.10 Muda safarini 0.40 – Muda wa kuondoka 3.30 3 + (60 + 10 – 40) 3.30 Alitoka kiamboni saa tatu unusu.