Maswali kadirifu

Zoezi A

a) Asubuhi moja nikielekea shuleni, kivuli changu kilikuwa mbele yangu.

Je, shule ilikuwa upande upi? __________

Nyumbani kwangu kulikuwa upande upi? _______

b) Jioni moja nikitoka machungani, kivuli changu kilikuwa upande wangu wa kulia, Je nilikuwa nikielekea upande upi?

c) Juma anaishi kusini mashariki ya Fatuma. Kwa hivyo Fatuma anaishi upande gani wa Juma?

d) Jua huzama upande upi? 

 

Zoezi B

a) Ni upande upi unaopatikana katikati ya kusini na magharibi?

b) Ni upande upi ulio katikati ya magharibi na mashariki?

c) Ni upande upi ulio katikati ya kaskazini mashariki na kaskazini?

d) Ni upande upi unaopatikana katikati ya kusini magharibi na magharibi?

e) Ni upande upi unaopatikana katikati ya kaskazini na mashariki?

Zoezi C

i). Jibu maswali yafuatayo ya dira

 

1. Kutoka Kusini mpaka Kaskazini Magharibi ni nyuzi ngapi?

2. Abi huishi suheli ya Kibi.Kibi anaishi upande geni wa Abi?

3. Jua hutua upande gani?

4. Jua Huchomoza janibu ya _____.

5. Taja mkabala wa Kusini Magharibi _____.

6. Wakati wa asubuhi kivuli huelekea upande gani?

7. Wakati wa jua la mkoche, jua huwa upande gani ?

8. Ikiwa shimali ni Magharibi, basi ___ ni matlai.

9. Upepo ulikuwa ukivuma kutoka Kaskazini matlai nasi tulikuwa tukienda dhidi ya upepo, kwa hivyo tulikuwa tukienda wapi?

10. Ni janibu ipi inayopatikana katikati ya Kusini na Magharibi?

 

ii). Chora dira huku ukionyesha pembe zote kumi na sita