Nasaba

- Nasaba pia inawezarejelewa kama ukoo.

- Nasaba ni uhusiano wa kizazi baina ya watu. Uhusiano huu unaweza kuwa katika familia au ukoo mmoja.

 

Mchoro: Uhusiano wa Kijamii

Majina ya ukoo/nasaba

1. Mama/nina: Mzazi wa kike.

2. Baba: Mzazi wa kiume.

3. Kaka: Ndugu wa kiume.

4. Dada: Ndugu wa kike.

5. Nyanya/Bibi: Mama wa baba au mama.

6. Babu: Baba wa mama au baba.

7. Mjukuu: Mtoto wa mwana.

8. Kitukuu: Mwana wa mjukuu.

9. Kilembwe: Mwana wa kitukuu.

10. Kilembwekeza/kining’ina: Mwana wa kilembwe.

 

11. Ami/amu: Kaka wa baba.

12. Shangazi/mbiomba amati: Dada wa baba.

13. Mjomba/hau: Kaka wa mama.

14. Halati/hale: Dada wa mama bila kubagua kama ndiye mdogo au mkubwa kwa mama yako mzazi. Pia huitwa hale.

15. Mkazahau: Mke wa mjomba.

16. Mkazamwana: Mke wa mwana au mke wa mtoto wako.

17. Mavyaa: Mzazi wa kike wa mume.

18. Bavyaa: Mzazi wa kiume wa mume wako.

19. Mamamkwe: Mama wa mke.

20. Babamkwe: Baba wa mke.

 

21. Mcheja: Mzazi wa mke au mume (mkwe).

22. Kivyere : Jina wazazi wa mume na wazazi wa mke hutumia kuitana.

23. Mpwa: Mtoto wa ndugu. Yaani unayemwita ami, shangazi, mjomba na halati naye atakuita mpwa.

24. Mkoi: Mtoto wa shangazi, mjomba, halati.

25. Binamu: Mwana wa kiume wa ami.

26. Bintiamu: Mwana wa kike wa ami.

27. Shemeji: Ndugu wa mke au ndugu wa mume.

28. Mama wa kambo: Mama asiyekuzaa lakini anakulea.

29. Baba wa kambo: Baba asiyekuzaa

30. Umbu: Jina waitanalo kaka na dada. Ni jinsi kaka anavyomwita dada naye dada anavyomwita kaka wakiwa wamezaliwa na mzazi mmoja.

 

31. Ndugu mlungizi: Ndugu anayekufuata

32.Ndugu mlungizi: Ndugu anayekufuata nyuma.

33. Wifi: (a) Mke wa kaka. Iwapo wewe ni msichana, mke wa kaka yako utamwita wifi. (b) Dada wa mume: Iwapo msichana ameolewa dada wa mumewe atamwita wifi.

34. Mwamu/mlamu: a) Kaka wa mke. Mwanamume akioa, kaka wa mkewe atamwita mlamu. b) Mume wa dada: mvulana au mwanamume atamwita mume wa dadaye – mlamu.

35. Mwanyumba: Ni mwanaume mwenzako aliyeoa kutoka boma moja ulikooa wewe. Ni mume wa dada wa mke wako.

36. Mkemwenza/mitara: Jina wanalotumia wanawake walioolewa na mwanamume mmoja.

37. Kifungamimba/ kitindamimba/ mzuwanda: Mtoto wa mwisho kuzali- wa katika familia.

38. Mwanambee/kifunguamimba/kichinjamimba: Mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia.

39. Nyanyamkuu: Mama wa nyanya.

40. Babamkuu: Baba wa babu.

 

41. Maharimu: Mtu usiyeweza kumwoa au kuolewa naye kwa sababu ya uhusiano wa nasaba.

42. Mnuna: Ndugu anayenifuata ndugu mdogo. 

43. Baba mkubwa - Ndugu wa kiume, mkubwa wa baba yako. 

44. Baba mdogo - Ndugu wa kiume, mdogo wa baba yako.