Maswali kadirifu

Zoezi A

Soma aya ifuatayo kisha ujibu maswali yatakayofuatia.

Pendo ni bintiye Fatuma na Hamisi. Pendo anao dada wawili: Subira na Baraka. Aidha, anaye kaka mmoja aitwaye Majaliwa. Pendo ameolewa na mwanamume aitwaye Rono. Wavyele wake Rono ni Kiprono na Nekesa. Rono anaye dada aitwaye Silvia na kaka aitwaye Musa. Rono na Pendo wamefanikiwa na mtoto aitwaye Eliza.

 

Jibu maswali yafuatayo:

1. Pendo na Silvia wataitanaje?

2. Eliza atamwitaje Fatuma?

3. Nekesa atamwitaje Fatuma?

4. Kiprono atamwitaje Eliza?

5. Subira atamwitaje Eliza?

6. Musa atamwitaje Pendo?

7. Pendo atamwitaje Kiprono na Nekesa?

8. Rono atamwitaje Fatuma na Hamisi?

9. Eliza atawaitaje kila mmoja wa hawa? a) Silvia b) Musa c) Majaliwa d) Baraka

10. Fatuma na Hamisi wataitanaje na Kiprono na Nekesa?

11. Rono na Majaliwa wataitanaje?

12. Iwapo Subira ana mtoto, Eliza atamwitaje mtoto huyo wa Subira?

Zoezi B

Jaza mapengo yaliyoachwa

1. Dadaye mjomba ni mama au

2. Mzazi wa kitukuu ni _________

3. Mzazi wa mkoi ni ________________

4. Babu au nyanya wa kilembwekeza ni ___________

5. Mke wa mwana ni ____________

 

Zoezi C

Jibu maswali yafuatayo

1. Musa na Fatuma ni ndugu. Fatuma ana mtoto aitiwaye Rosa. Je, Rosa atamwitaje Musa?

2. Karembo na Kazuri ni dada wa toka nitoke. Karembo ameolewa na Vumilia naye Kazuri ameolewa na Stahamala. Je, Vumilia na Stahamala wataitanaje?

3. Tumaini na Neema ni ndugu wa toka nitoke. Nyanya yao anaitwa Baraka. Je, Tumaini na Neema wataitwaje na Baraka?

4. Meho amemwoa Susi. Mamaye Meho anaitwa Pendo. Pendo atamwitaje Susi?

5. Kali anaye dada aitwaye Mpole. Mpole ameolewa na Tarajio. Tarajio na Kali wataitanaje?

6. Kakaye mama huitwaje?

7. Ndugu wa kike wa mama huitwaje?

8. Kaka yake mama anaitwa Bora. Ana mke aitwaye Tuishi. Je, nitamwitaje Tuishi?

9. Pale na Hapo ni ndugu. Hapo ana mtoto aitwaye Leo. Pale atamwitaje Leo?

10. Mjukuu wa kitukuu ni nani?