Maswali kadirifu

A. Jibu maswali yafuatayo kwa kuteua majibu sahihi.

Viteuzi: buibui, kanchiri, chepeo, tarbushi, kisutu, dangarizi, sare, shimizi.

 

1. Wanawake wa Kiislamu huvaa vazi jeusi juu ya nguo zaoza kawaida. Vazi hilo huitwa _____.

2. Nguo za wanafunzi shuleni huitwa _____.

3. Vazi linalovaliwa ndani ya rinda na wanawake huitwa _____.

4. Suruali ndefu iliyoshonwa kwa kitambaa kigumu aghalabu cha rangi samawati huitwa ____.

5. Kivazi kinachovaliwa na wanawake vifuani ili kusetiri dodo huitwa _____.

6. Kofia ya 'samahani jua' pia huitwa _____.

7. Kanga ambazo zimetiwa nakshi ya kila aina huitwa _____.

 

B. Je, kina nani huvaa mavazi haya?

Mfano: sharti - wanaume     kocho - wote

            blauzi - wanawake    ubinda - watoto

1. kaniki           2. gaguro

3. kirinda          4. seruni

5. fulana           6. pajama

7. bwelasuti      8. suruali

9. bombo          10. shimizi

11. mahazamu  12. shali

13. kanzu         14. buibui         15. kikoi