Hadithi  by  Joab Otieno

6

Hadithi ni nini?

Hadithi  ni utungo wenye visa vya kubuni unaosimuliwa kwa lugha nathari kwa kusudi la kuburudisha, kukuza maadili na kuunganisha jamii.

Jina lingine la hadithi ni nini?

Ngano

Ili kusimulia hadithi msimulizi huzingatia nini?

Vianzio

Soma vianzio hivi

Hapo zamani za kale.................
Hapo zamani za konga mawe...........
Miaka na dahari......................
Zama za zama...............................
Hapo jadi na jadudi..............................
Ewe!ningependa kulikunjua gayagaya(jamvi) hili kwa kwenda sambamba kama samaki na maji na wakale kuwa...................... 

Msimulizi aweza kuanza vipi?

Soma kinogezi hiki.

•Paukwa! pakawa! Sahani na kawa,baiskeli ya watu wote,giza la mwizi,kiboko cha mtoto mkorofi na maziwa ya moto.
•Hapo.................

Sikiliza kwa makini kinogezi hiki.

[resource: 6053, align: left]

ZOEZI

•Andika Insha bora kuhusu
•''Hadithi niipendayo''