Ufahamu: Binadamu na wanyama  by  Olpha Janduko

6

   Hapo jadi wakati binadamu,wanyama na ndege walikuwa wanaongea lugha moja na walikuwa marafiki wa kufa kuzikana, hakukuwa na mauti wala uwele kwa hivyo walikuwa wanaishi kwa furaha na amani.

Wakati mmoja ndoto ilimjia binadamu katika usingizi.Na ndotoni alisikia ikisema,"ewe mwanadamu,"kwa sauti kakamavu."Sikilizeni na utilie maanani haya maelezo yatakayotegemea uamzi wako".
Muda si muda mwanadamu aligutuka kutoka usingizini na kusikiliza,"kuna uamuzi unatakikana kufanya na uamuzi utakaoufanya utadumu milele. Kwa kuwa wewe ni mwerevu kuliko wanyama wengine,sasa inafaa uchague kati ya mwezi na wanyama pia ndege ni nani atakufa apotee au afe na afufuke".
   Baada ya kufikiria akasema,"wacha niende nipate wosia kutoka kwa viumbe wahusika kesho nikakupe jawabu sahihi".Usiku huo binadamu hakupata hata lepe la usingizi,aliyawaza maneno aliyoyasikia. Kulipokucha binadamu aliwaita wanyama na ndege ili awaeleze yaliyojiri usiku huo.Wanyama na ndege waliitikia mwito maana mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.
   Bila kupoteza wakati,binadamu aliwasabahi  kwa heshima na baada ya salamu akawashukuru kwa kuitikia wito wake,akaendelea,"nijiwa na sauti ndotoni  ikinipa mambo mawili ili nifanye uamuzi".Wanyama na ndege walishikwa na butwaa. "Wenzangu niliambiwa niamue kati ya wanyama,ndege na mwezi atakayekufa afufuke na atakayekufa apotee".Wanyama na ndege walimwabia akaseme kuwa mwezi ufe upotee na wanyama na ndege wafe wafufuke na wakaagana.

6

   Usiku ulipofikaa,ile sauti ilimjia binadamu na kumuuliza atoe jibu.Naye akajibu"mwezi ufe upotee wanadamu na ndege wafe wafufuke."Ile sauti ikasema,"naam, ni jawabu nzuri lakini utawawakilisha wanyama na ndege mbele ya Mwenyezi Mungu."Binadamu aliachwa kinywa wazi baada ya kuyasikia hayo maneno. Pindi tu ile sauti ikamwaagiza aende akwee mlima na akifika kileleni apige magoti na kusema,"Ewe Mwenyezi Mungu kwa niaba ya wanyama na ndege,ninaomba mwezi ufe upotee ba wanyama na ndege wafe wafufuke." Asubuhi ilipofika binadamu alienda kuukwea mlima.alipofika alianza kukwea mlimani lakini haikuwa  kazi rahisi kwake,alitamani kurudi nyumbani.Alijikaza kisabuni mwishowe akafaulu,alipofika kileleni chini angalau apumzike.

   Muda si mrefu usingizi ulimchukua,akalala fo fo fo kwa muda mrefu.Alipogutuka alikuwa amesahau yale maneno aliyotakikana kutamka. Binadamu aliwaza na kuwazua,baina ya kurudi au kufikiria kwa makini angalau akumbuke hata neno moja.Licha ya hayo aliona kuwa akirudi nyumbani bila kufanya alichohitajika atadharauliwa na wanyama wengine. Baada ya kufikiri kwa makini,aliyakumbuka na kwa vile muda ulikuwa umeenda ,alianza kutamka bila kujipanga,"mwezi ufe ufufuke wanyama na ndege wafe wapotee.alipojirudia na kufikiria vizuri,alianza kujilaumu.Ndio maana mwezi unakufa na kurudi ilhali viumbe wenye uhai wanakufa na kupotea.

6

Maswali.

1.Neno kufa kuzikana ni fani gani ya lugha?
(A) Semi
(B) Methali
(C) Kitendawili
(D) Istiara
2.Toa kisawe cha neno uwele.
(A) Shida
(B) Mzee
(C) Ugonjwa
(D) Amani
3.Lengo kuu la binadamu kuwaita wanyama na ndege mkutanoni ni?
(A) kuwaalika karamu
(B) kuwasihi waitikie wito
(C) kuwatuma waende mlimani
(D) kuwauliza maoni yao juu ya sauti iliyomjia ndotoni
4.Kujikaza kisabuni kulingana na ufahamu inamaanisha
A) kujitolea kufanya jambo ili ufanikiwe
(B) kununua sabuni
(C) kutumia sabuni kufulia
(D) kuchoka
5.Kulingana na ufahamu chaguo lilikuwa kati ya:
(A) binadamu kukwea mlima
(B) wanyama, ndege na mwezi
(C) binadamu na mwezi
(D) wanyama na binadamu
6.Ni jawabu gani wanyama na ndege walilompa binadamu?
(A) Mwezi ufe upotee,wanyama na ndege wafe wafufuke
(B) Mwezi ufe upootee,wanyama wafe wafufuke
(C) Mwezi ufe upotee,ndegee wafe wafufuke
(D) Mwezi ufe upotee,binadamu afe afufuke
7.Binadamu alitumwa kuwawakilisha wanyama na ndege mbele ya nani?
(A) ya mlima
(B) ya wanyama
(C) ya Mungu
(D) ya mwezi
8.Binadamu alifanya nini alipofika kileleni mwa mlima?
(A) Alioga kwa sabuni
(B) Aliyatamka yale maneno
(C) Alimwita Mwenyezi Mungu
(D) Alikaa kupumzika usingizi ukamchukua
9.Ni nani aliyesababisha kifo?
(A) Mwenyezi Mungu
(B) Ndoto
(C)  Binadamu
(D) Mwezi
10.Chagua kichwa mwafaka cha ufahamu huu.
(A) Binadamu na kifo
(B) Mwezi na kifo
(C) Chanzo cha kifo
(D) Mlima wa kifo

Majibu

1  (A) Semi.
2. (C) Ugonjwa.
3. (D) Kuwauliza maoni yao juu ya sauti iliyomjia ndotoni.
4. (A) Kujitolea kufanya jambo ili ufanikiwe.
5. (B) Wanyama,ndege na mwezi.
6. (A) Mwezi ufe upotee,wanyama na ndege wafe wafufuke.
7. (C) ya Mungu.
8. (D) Alikaa kumpumzika usingizi ukamchukua.
9. (C) Binadamu.
10.(C) Chanzo cha kifo. 



  • 0202fb8a-8736-49d9-93de-f47de26c0054 by elimu used under CC_BY-SA
  • 3aad2000-c203-4ea2-982d-9176c581641c by elimu used under CC_BY-SA
  • 4a88cf55-8222-49ba-9236-8a85ab44ef99 by elimu used under CC_BY-SA
  • 7bddc84c-eb67-4f99-aaeb-095e52e70acf by elimu used under CC_BY-SA
  • 0959a4f7-66a5-40d4-856a-cf042b21749b by elimu used under CC_BY-SA
  • 186b8594-515f-4592-9235-9271c9754b0b by elimu used under CC_BY-SA

  • Creative Commons License
    All work unless implicitly stated is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial-NoDerivatives 4.0 International License.