Matumizi ya ‘ote’  by  Margaret Nguli

6

Ote ni kivumishi cha kutaja jumla au pamoja au kitu kizima bila kugawanya au kutengganisha. Mfano mlo wote au jumba lote, ina maana kuwa pamoja au jumla au mzima bila kuacha kingine kando.

Mifano katika sntensi

  • Nguo yote ilichafuliwa.
  • Chakula chote kililiwa.
  • Jumba lote lilisafiswa.
Ote hutumika kuonyesha kati ya vingine au miongoni mwa. Vitu kadhaa wala si vyote.
Baadhi tu, bila kuchagua wala kubagua.

MIFANO KATIKA SENTENSI

  • Mwanafunzi yeyote anaitwa na mwalimu.
  • Chochote kiingiacho mjini si haramu.
Vivumishi ote na o--ote huchukua kiambishijina hivyo huchukuana na ngeli husika kwa mwingiliano thabiti.

ZOEZI

  • Fujo ____ za kisiasa hazifai kamwe na zinafaa kuzikwa katika kaburi la sahau.
  • Ukimwi ni uwele mbaya kwa mja ____.
  • Watu wakiishi bila mpaka ____ wa maisha, watakuwa pakashume
  • Ajira ____ kwa watoto hafai.
  • Mitume _____ watakuwa na mkutano wao kesho.

MAJIBU

  • Zozote
  • Yeyote
  • Wowote
  • Yoyote
  • Wowote