Matumizi ya 'ji'

Silabi ji hutumika kwa njia nne:

  •  ji- ya nafsi Hutumika mtendaji anapojirejelea k.m Nilijiuliza maswali mengi kuhusiana na maisha yangu.

  •  ji ya mtendaji Huwekwa mwishoni mwa neno kuashiria anayetenda jambo k.m. Anayesoma ni msomaji. Anayeruka ni mrukaji.
  • ji ya ukubwa Huwekwa mwanzoni mwa baadhi ya nomino kuashiria hali ya ukubwa. k.m. mtu – jitu, mbwa – jibwa.

  • ji ya kuonyesha hali k.m. Uogeleaji wake ulivutia.