Matumizi ya 'karibu'

Matumizi ya karibu

Karibu hutumika kwa njia mbalimbali:

1. Karibu ya masafa (umbali) k.m Tunaishi karibu na soko.

2. Karibu ya makaribisho k.m. Tulipobisha hodi, mwenyeji alitujibu, “karibu”.

3. Karibu ya kiasi (idadi). k.m. Alikula karibu matunda ishirini.

4. Karibu ya kitendo kukaribia kutendeka (karibu ya nusura) k.m. Karibu mwogeleaji huyo aibuke mshindi.